Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Dk. Magufuli "amponza" Halima Mdee ..... Mdee atakuwa kukamatwa Mara mojaMkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ametoa agizo la kukamatwa kwa Mbunge Halima Mdee mara moja kwa kosa la kumkashifu Rais John Magufuli.

DC HAPI AAGIZA MBUNGE HALIMA MDEE AKAMATWE Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi ameliagiza jeshi la Polisi Kinondoni kumkamata Mbunge wa Kawe Halima Mdee kwa kosa la kutoa kauli za matusi, dhihaka na uchochezi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi kwa ujumla. Hapi ameagiza mbunge huyo kukamatwa, kukaa korokoroni kwa saa 48, kuhojiwa na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kwa maneno aliyoyatoa jana akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema mtaa wa ufipa. Hapi amesema kuwa maneno aliyoyatoa Mdee ni matusi yenye lengo la kuleta uchochezi unaoweza kuhatarisha amani na utulivu. "Sitamvumilia mwanasiasa yeyote atakayethubutu kutoa kauli za matusi dhidi ya Mh. Rais, au zenye kutaka kuleta uchochezi katika wilaya yangu." Alisema DC Hapi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top