Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza John Nzwalile amesema amehama Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwasababu ana njaa na kiu ya maendeleo kama inavyosimamiwa na Rais John Magufuli anayetetea maslahi ya Taifa .
Amesema kama tatizo lilikuwa ni kumpata kiongozi jasiri na mzalendo anayeweza kupigania maendeleo na maslahi ya umma, Rais Magufuli anatosha, anafaa na katu hastahili kupingwa.
Nzwalile aliyaeleza hayo jana wakati mbele ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM shaka hamdu shaka aliporudisha kadi ya Chadema akiwa na wenzake 30 katika mkutano wa ndani uliofanyika kwenye Uwanja wa wa CCM Kirumba Mkoani hapa.
Alisema kitendo cha Rais Dk Magufuli ndani ya kipindi cha miaka miwili cha utawala wake kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo, ndicho kilichowashawishi hadi kufikia uamuzi huo si vinginevyo.
"Kuna watu wanasema tumehamia ccm kwasabau ati tuna njaa, niseme kweli sisi hatuna njaa ya kula wala kulala, shida na njaa yetu ni aina ya maendeleo yanayopiganiwa na Rais Dk Magufuli" Alisema
Aidha Nzwalile alimuonya Mwanasheria wa chadema na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (chadema ) kuacha kuitolea maneno ya dhihaka na kejeli serikali inayoongozwa na Rais aliyewekwa madarakani kwa mujibu wa katiba.
Alisema maneno anayotamka Lissu huenda si msimamo wa Chadema ila yametoka katika kinywa cha mwanasiasa anayekabiliwa na msongo wa mapepo na ushetani hivyo anahitaji kuombewa hatimaye anusurike .
Nzwalile alisema Lissu hana ubavu wala misuli ya kushindana na serikali kwani yeye ndiye iliyekamata mpini na Lissu ameshika makali hivyo asitegemee kupata ushindi kwa kutoa maneno ya kejeli.
Licha ya Nzwalile kurejea ccm, wenzake wengine aliorudisha nao kadi toka chadema katika shina la Nyehunge kata ya Kirumba wilayani Ilemela.
Kuhama kwa wanachama hao katika shina la Nyehunge kurudi ccm kumesababisha kuvunjika kwa kijiwe cha chadema.
End
End
Post a Comment