Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Shaka awatolea uvivu Maafisa kilimo na mifugo



Na Mwandiahi Wetu, Mwanza
Wakurugenzi wa halmshauri za wilaya wametakiwa kuwaelekeza maafisa wa kilimo, ufugaji na maendeleo ya ustawi wa jamii kutokaa maofisini badala yake wayafuate makundi ya wajasiriamali wakiwemo wakulima na wafugaji kuwaelimisha na kuwafundisha kitaalam.
Pia wataalam wote wametakiwa kutimiza majukumu yao bila kusubiri kusukumwa na mtaalam atakayeshindwa kuwajibika katika idara yake hapaswi kubaki kama muajiriwa katika halmashuri husika.
Ushauri huo umetolewa na Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka alipokitembelea kikundi cha kilimo cha umwagiliaji cha kata ya sangabuye kinachojishuhulisha na kilimo cha bustani na mbogamboga kando kando ya Ziwa Victoria .
Shaka alisema ni wajibu usiokwepeka kwa kila wataalam wa kilimo kuendelea kuyatazama kwa macho maji ya Ziwa Victoria bila ya kuyatumia katika kilimo cha umwagiliaji ambacho kinaweza kuzalisha ajira nyingi kwa vijana.
Alisema inasikitisha kuona bado hakujawa na nguvu nyingi zitokanazo na utaalam wa maafisa wa kilimo katika kuweka umuhimu na mkazo kwa halmsahuri zote ambazo ziko karibu na maziwa pamoja na mito zisifanye kilimo cha umwagiliaji.
"Tuna maafisa wamemaliza masomo yao katika fani za kilimo, ustawi wa jamii na mifugo, wamepata ajira, najiuliza ni lini wataanza kuonyesha matunda ya taaluma zao. tuna ardhi, siasa safi, uongozi bora, sera, watu na zana za kilimo .tunashindwa wapi?" Alihoji Shaka
Alisema hata kukua kwa maendeleo ya viwanda yanahitaji kupata msukumo wa mazao yanayozalishwa aidha yatokanayo mashambani katika kilimo au kwenye mifugo ya wanyama mbalimbali, mistu, maziwa na bahari na vitu vingine.
Shaka akimpongeza mbunge wa Ilemela Angelina Mabula kwa utayari wake wa kuwayakusanya makundi ya vijana kuwahamasisha, kuwapatia baadhi ya zana za kujiendeleza katika shughuli za kilimo.
"Maji haya ziwani ambayo ni zawadi toka kwa mungu hayajatumika ipasavyo, yakitumika yataongeza wigo ajira katika sekta ya kilimo, kila binadamu anahitaji kula, anataka mbogamboga, nafaka, matunda katika maisha yake, kilimo hakimtupi mtu"Alisema kaimu huyo katibu.
Aliwataka vijana kutopoteza muda wao bure kwa kupiga maneno mitaani badala yake wajikusanye pamoja na kushiriki kuanzisha miradi ya kiuchumi kulingana fursa zilizopo katika maeneo yao ikiwemo nyanja za kilimo, biasahara, ufundi na uvuvi.
Hata hivyo kaimu katibu mkuu aliwataka wana kikundi cha kilimo Sangabuye kutokata tamaa badala yake waendelee na mikakati ya kufikia malengo yao kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa njia halali.
"Mmeanzisha mradi huu ambao ni muhimu sana kimaendeleo. nitakutana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela nitamuelezea nilichokiona, hapa mnafanyakazi na wala hamfanyi mchezo mchezo, nyinyi mnahitaji kusaidiwa kwa kila hali kuunga mkono jitihada hizi za kujituma na kutaka kuinua kipato chenu "Alieleza
Msafara wa Shaka toka eneo la mradi ulielekea moja kwa moja katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ilemela ambapo ulikutana na Kaimu Dc wa wilaya hiyo Neema Kipeja ambaye ni Afisa Tawala wa wilaya ya Ilemela kabla ya kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa halmshauri ya wilaya Ilemela huko akazungumza na madiwani pamoja na wakuu wa idara.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top