Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Panga pangua Polisi

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo 
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro,  amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna  Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Salome Kaganda amekuwa Mkuu wa kitengo cha Mafao na Fidia  Makao Makuu ya Polisi, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo ambaye alikuwa kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga.

Aidha, Nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Sylverius Haule, ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu  wa Polisi wa Mkoa wa Mara.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya  Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Imetolewa na:
Barnabus D. Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top