Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Shaka azidi kutikisa Kigoma





















*YALIYOJIRI LEO JUMANNE 18/07/2017 KATIKA ZIARA YA KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC) MKOA WA KAIGOMA WILAYA YA KIGOMA MJINI NA KIGOMA VIJIJINI*

*WILAYA YA KIGOMA MJINI*

- Amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa mashina na matawi wapya waliochaguliwa, kata na wilaya ya Kigoma mjini wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika ukumbi wa mikutano  Kizito Kigoma mjini.

- Ametembelea na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, kikundi cha vijana wanaojishuhulisha   mradi wa uwekezaji viwanda vidogo vidogo utengeezaji sabuni na usimikaji wa dagaa katika kata ya  Mwanga

- Amezungumza na wanachama wa CCM na jumuiya zake, wazee waasisi,  wakinamama na vijana ofisi ya kata ya Gungu    na kisha kushiriki ujenzi wa Taifa wa ofisi ya kata hiyo  ambalo lilijengwa mwaka 1962-1963  na sasa linafanyikwa ukarabati mkubwa.

- Hadi kukamilika kazi ya ujenzi wa ofisi hiyo ya kata jumla ya T. Shs 2,094,500 zinahitajika ambapo  Kaimu katibu  Mkuu amendesha  harambee ya papo kwa papo na jumla ya T. shs  355,000/= taslim  zilikusanywa  na vifaa vyenye thamani ya T.shs 1,160,000/= vilichangwa ili kukamilisha ujenzi huo.

-Ametembelea eneo la uwekezaji la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kigoma ambalo taratibu zimekamilika kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha uwekezaji cha  biashara.

*WILAYA YA KIGOMA VIJIJINI.*

-Pamoja na viongozi aliofatana nao wameshiriki katika ufyatuaji wa matufali katika kikundi cha  Mgera Youth Group katika kata ya Mwandinga cha  wajasiriamali  wanaojishuhulisha na  shuhuli mbali mbali za uzalishaji zinazofanywa ikiwemo kufyatua tufali za kuchoma, kutengeneza sabuni, uvuvi na mradi wa visa kilichoanzishwa mwaka 2015.

-Mbunge wa viti maalum Vijana Mkoa wa Kigoma Zainab Katimba  amewachangia wanakikundi hao vyarahani 5 na Kaimu Katibu Mkuu amewachangia Fedha taslim kuchangia mfuko wao wa hisa  cha kuweka na kukopa cha vijana hao.

-Amezindua shina la wakereketwa na kisha kuzungumza na vijana  kundi kubwa la vijana katika kata ya Kagongo kijiji cha Mgaraza ambapo pia aliwapokea viongozi 19 waandamizi wa wilaya na kata toka katika vyama vya upizani   vya CUF, ACT wazalendo na NCCR Mageuzi ambao aliwakaribisha na kuwakabidhi kadi za CCM.

-Ametembelea na kushiriki kazi ya uchimbaji msingi kwa ajili  ya usambazaji wa maji safi na salama katika kijiji cha Kalinza na Mlagala  ikiwa  ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM 2015/2020 mradi ambao utagharimu T.shs  786,642,000/= Fedha zinazotoka katika Mfumo Mkuu wa Serikali.

-Wakati huo amekabidhi kadi kwa wanachama wa CCM na jumuiya zake waliotimiza masharti ya uanachama  kikatiba na kikanuni  kama ifuatavyo:-      
CCM 591
 UVCCM 482
 UWT  82 na
WAZAZI 62

Ziara ya  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) itaendelea kesho katika wilaya ya Buhingwe na Kasulu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top