Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UVCCM waukwepa 'mtego' wa kupanga safu

Na Mwandishi Wetu, Nyamagana-Mwanza
Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesema kuwa hauwezi kufumbia macho wanachama wa jumuiya hiyo walioomba nafasi Mbalimbali za kugombea ilihali wanajiimarisha katika safu za kisiasa.
Umoja huo umesema kuwa kupanga safu katika chaguzi Mbalimbali za Chama ni makosa makubwa kwa wagombea na hata wanachama wasiokuwa wagombea kwani kufanya hivyo ni kukiuka Mpango madhubuti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuimarisha nchi katika sekta ya  kiuchumi na kijamii kupitia CCM Mpya na Tanzania Mpya.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo Julai 25, 2017 Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza Wakati wa ziara ya siku moja alipokuwa akizungumza na Vijana wa Jumuiya ya Chama hicho (UVCCM) pamoja na  wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mara baada ya kufungua shina la wakereketwa Eneo la Stendi ya Mwaloni maarufu kama Mererani.
Shaka alisema kuwa Jumuiya ya Vijana ni Jeshi mahususi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo kuelekea uchaguzi Mkuu wa Chama na Jumuiya zake CCM imejipanga kuwapata viongozi madhubuti watakaoweza kuimarisha usawa katika jamii na Kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Mwaka 2015-2020.
Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM Kimepewa dhamana kubwa na Wananchi  ya kuwaletea maendeleo hivyo kufanya mikutano ya ndani nchini ni sehemu ya kuangalia namna utekelezaji wa Imani waliyoitoa Wananchi kupitia ilani inavyosimamiwa.
Shaka amewasihi Wananchi kutoa ushirikiano Mkubwa kwa madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ili kutimiza ndoto ya Tanzania ya maendeleo endelevu.
Katika Ziara hiyo Kaimu Katibu Mkuu huyo ameshiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Bugarika Kaskazini na kuahidi kumalizia katika upauaji jambo ambalo limemfanya pia Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula kuchangia Bando tatu za bati ili kumuunga mkono Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka.
Aidha, Shaka ameshiriki ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha Mawe yenye urefu wa Kilomita moja kwani itatoa urahisi wa Huduma za kijamii hususani kwa Wakati wa Kaya ya Mahina na Kata ya Pamba.
Alisema kuwa tayari Vijana wengi wamepata ajira kwenye ujenzi huo na kujipatia kipato kizuri kinachoanzia shilingi 28,000 mpaka Shilingi 40,000 kwa siku.
MWISHO
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Bugarika Kaskazini Wakati wa Ziara ya kikazi Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akimsalimu Mlemavu anayeomba katika eneo la Mtaa wa Pamba-Posta Wakati wa Ziara ya kikazi Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mheshimiwa Stanslaus Mabula akizungumza mara baada ya ufunguzi wa Tawi la UVCCM katika Stendi ya daladala Mwaloni maarufu kama Mererani, uzinduzi huo umefanywa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Wakati wa Ziara ya kikazi Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mheshimiwa Mary Tesha akizugumza mara baada ya ufunguzi wa Tawi la UVCCM katika Stendi ya daladala Mwaloni maarufu kama Mererani, uzinduzi huo umefanywa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Wakati wa Ziara ya kikazi Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akishiriki ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha Mawe Wakati wa Ziara ya kikazi Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana  UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) katika Picha ya pamoja na viongozi wengine wa Chama akiwemo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula Mara baada ya kushirikiana ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Bugarika Kaskazini
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top