Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wanafunzi 10 wafutiwa matokeo kidato cha sita 2017

Wakati matokeo ya mitihani ya kidato cha sita yakitolewa leo, Jumamosi Julai 15, imebainika kuwa watahiniwa 10 walifutiwa matokeo kwa makosa ya kufanya udanganyifu.

 Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta),  Dk Charles Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.

 Pamoja na hao kumi, matokeo ya watahiniwa wengine 15 yalizuiliwa kwa kuwa hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo.

 Watahiniwa hao walishindwa kufanya mitihani kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya baadhi ya mitihani hiyo.

‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama wa watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde.

Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top