Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli alivyotikisa uchaguzi wa Kenya



GUMZO LA JPM UCHAGUZI WA KENYA

Uchaguzi Mkuu wa Kenya 🇰🇪 umefanyika siku ya Jumanne Agosti 8, 2017 ambapo kulikuwa na mchuano mkali kabisa kati ya Uhuru Kenyatta mgombea wa Jubilee na Raila Odinga mgombea wa NASA ambapo matokeo yanaonyesha Uhuru Kenyatta kumzidi Odinga kwa asilimia 10 ya matokeo mpaka sasa.

Uchaguzi wa Kenya umeshirikisha jumla ya wagombea 8 waliokuwa wanawania kiti cha urais.

Mchuano ulikuwa mkali sana na tangu mwanzo kulipoanza kampeni ambapo jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿 Dkt.John Pombe Magufuli lilitawala sana. Kwa upande wa wagombea Urais jina la Dkt. Magufuli lilitawala na kuwa gumzo kwenye kampeni zao kwa zaidi ya asilimia 98, si Odinga wala si Kenyatta wote walikuwa wakimtaja Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli mara kwa mara kabla hawajashuka majukwaani.

Utawasikia,"Tunataka mabadiliko kama yanayotokea Tanzania ya kupambana na wezi na ufisadi katika serikali ya Magufuli", wengineo utawasikia,"Nikishinda nitaongoza nchi kama Magufuli ". Yaani lilikuwa linapotajwa jina la Magufuli uwanja mzima  unalipuka kwa shangwe.

Inawezekana kabisa kushinda kwa Kenyatta ama kutikisa kwa Odinga na kuleta ushindani mkali na wa dhahiri kunatokana na wote wawili (Uhuru na Odinga) kusafiria nyota ya Rais Magufuli wakati wa kampeni ambaye alikuwa nyota ya uchaguzi wa Kenya.

Kung'ara kwa Rais Magufuli kwenye siasa zinatokana na ukweli Wakenya wengi wanampenda mno Rais Magufuli kwa namna anavyoienda nchi yake Tanzania 🇹🇿.

Wakenya wengi wanavutiwa na Rais Magufuli kwa namna anavyopambana na rushwa na ufisadi Serikalini ambao umekuwa kero Kubwa kwa Wakenya wengi ambao kiwango cha rushwa na ufisadi ni kikubwa mno wanatamani wangempata Magufuli awasaidie kuondoa tatizo hilo.

Wakenya wanavutiwa na namna ambavyo Rais Dkt. Magufuli anavyotengeneza fursa za ajira nchini kwa kuhakikisha viwanda vingi vinaanzishwa, kilimo kinaboreshwa, kuwaondoa maofisini wenye majina na vyeti feki wanaoziba fursa za wenye vyeti halali. Wakenya wengi sana ni wasomi lakini wengi wao hawana ajira, wanamtamani Magufuli awatengenezee fursa za ajira.

Wakenya wanavutiwa na Magufuli kwa namna anavyotetea rasilimali za Taifa zimnufaisha Mzawa husika na si mwekezaji au mgeni. Uzalendo wa Rais Magufuli katika kulinda rasilimali za nchi ya Tanzania zimewafanya Wakenya wengi kuzidi kuongeza mahaba kwa Rais Magufuli.

Wakenya wengi wanampenda Rais wa Tanzania 🇹🇿 Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyotekeleza Ilani ya uchaguzi kwa kusimamia kauli zake nyakati za uchaguzi.

Wakenya wengi wanavutiwa na Rais Magufuli kwa namna alivyoboresha nidhamu na uwajibikaji kwa Watumishi wa umma.

Kiukweli kila mgombea aliyesafiria nyota ya Rais Magufuli ameonekana kupata kura za kutosha za kushinda na wengine kuleta ushindani mkali kabisa.

Jina la Dkt.Magufuli sio tu lilikuwa likitumika Kenya bali hata kwenye Uchaguzi wa Rwanda, wametumia sana jina la Rais Magufuli wakati wa kampeni.

Mnyonge, mnyongeni haki yake mpeni. Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekuwa nyota na kipenzi cha walio wengi kwa uzalendo, uchapa kazi, usimamizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM).

Majalida mbalimbali Afrika na Duniani wamekuwa wakimtaja Rais wa Tanzania Dkt.Magufuli kama Kiongozi wa Mfano barani Afrika.

Na Emmanuel J. Shilatu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top