Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Shein aagiza apewe majina ya Vigogo wa ardhi wasio waadilifu awatumbue

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amemtaka mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi kuwatafuta na kumpelekea majina ya viongozi wanaosababisha migogoro ya ardhi katika mkoa huo haraka iwezekanavyo.

Agizo hilo amelitoa leo wakati akitamatisha ziara yake ya siku 3 iliyoanza juzi Ijumamosi mkoani humo, ambapo amesema moja ya mambo aliyokutana nayo ni pamoja matatizo ya ardhi ambayo yanasababishwa na viongozi wabadhirifu na kuagiza watafutwe na apatiwe majina yao ili ashughulike nao maramoja

Mbali na agizo hilo, Rais Shein pia amemuagiza Mkuu wa mkoa huo Ayoub Mohamed Mahamoud kushgulikia masuala kadhaa ikiwemo Wizi, Msongamano wa magari, Kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watumiaji wote, kukumbusha tatizo la Ukimwi kuwa bado lipo, Usafi wa masoko, Gari zisiingie katikati ya mji mkongwe bila utaratibu.

Hata hivyo Rais Shein amefurahishwa na namna mkoa huo chini ya RC Ayoub Mohamed Mahamoud ulivyotekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi kubwa.

Rais Shein alianza ziara yake siku ya Ijumamosi katika wilaya ya mjini, Siku ya Ijumapili alizuru wilaya ya Mjini magharibi 'A' na leo siku ya Ijumatatu amemalizia katika wilaya ya Magharibi 'B' mkoani humo ambapo alikagua na kuzindua miradi ya maendeleo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top