Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MASHA AMEKWEPA UPUUZI, KITILA AMEKATA MZIZI WA FITINA



Baadhi ya viongozi, wasomi magwiji na wachambuzi nguli wa masuala ya kisiasa mara kadhaa wamekuwa wakisema kuwa kubaki ndani ya Chadema kunahitaji maarifa haba,  akili fupi na uwezo mdogo wa kufikiri au kupima na kupambanua mambo .

Wanasema hivyo wakidai  ndani ya chama hicho kumekosekana  mpango  mkakati wa kukijenga chama hicho na kuonekana  ni taasisi halisi ya kisiasa yenye kuchukua juhudi ya kusaka amana, imani ili kuaminiwa na wananchi au kuvuna kura kwenye uchaguzi Mkuu.

Wadadisi wa mambo ya siasa wanabainisha kuwa ndiyo maana hadi sasa Mwanasiasa Mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amekataa katakata kutangaza kama amejiunga na Chadema licha ya kujitoa CCM  nyakati za kampeni za uchaguzi Mkuu .

Mzee Ngombale inadaiwa tokea awali akiwa CCM amewahi kukiponda chama hicho na mara kadhaa amenukuliwa akisema  hakijatokea chama chenye mfumo wa kisiasa, chenye sera mwanana, oganaizehsheni na miongozo bora.

Mwanasiasa huyo amekipima chama hicho, kukichambua na wakati fulani licha ya kutokuwa mwanachama halisi, amekuwa akimshauri Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akitaka wajiondoe na kutoonekana chama cha kiharakati ili kuwa taasisi kamili.

Ujio  wa Waziri wa zamani wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwanasheria Lawrance Masha ndani ya Chadema ulisukumwa na hamaki, tamaa ya fahari ya macho kwenye mikutano ya hadhara ya Chadema hatua ambayo inatajwa kuchangia kumpa matumaini hewa na kutaraji pengine Chadema kingeshinda na kuchukua dola.

Mara kadhaa Masha kwa kutumia usomi wake, upana wa maarifa, uzoefu katika siasa na uongozi kila alipojitutumua na kushauri alibezwa, kukwepwa huku baadhi ya wanasiasa wenye uoni mdogo na muhafidhina wakimtenga na kumpuuza.

Wiki mbili kabla ya kufikia uamuzi wake Masha alikuwa na mazungumzo marefu na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa na kumueleza kuwa amefikia maamuzi ya kujiondoa chadema na kufanya shughuli zake binafsi.

Yapo maelezo kuwa Lowasa alimbembeleza na kumsihi sana Masha abatilishe msimamo wake na kutaka awe mwenye subira kwani si muda mrefu chama hicho kitabaki mikononi mwao huku kina Mbowe na washirika wake watakalia benchi kwasababu wameshindwa siasa za mapiku na ushindani.bMasha alimkatalia katakata Lowassa na kusema amechoshwa na upuuzi

Kwa upande Prof Kitila Mkumbo amepitisha maamuzi rasmi ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi akiwa Mkoani Singida. Amekuwa mpinzani kwa miaka mingi akitokea Chadema ambapo alikuwa Mshauri Mkuu na Mjumbe wa Kamati kuu.

Piia amewahi kuwa mshauri mkuu na muasisi wa ACT Wazalendo. Profesa Kitila alijiondoa Chadema akiwa na kina Samson Mwigamba, Habib Mchange na Zitto zuber Kabwe baada ya kuzuka mizengwe na kutoridhishwa na mwenendo wa Chadema.

Prof Kitila atakumbukwa kwa uandikaji makala zenye fasihi huku akizibebesha ujumbe wenye muwala  pia kuandaa ilani ya uchaguzi ya Chadema ya uchaguzi wa mwaka 2010 iliyomnadi mgombea urais wa chama hicho wakati huo Dr Wilbroad Slaa.

Wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya  siasa wanadai Chadema hakijawahi kuwa na Ilani ya uchaguzi 'realistic , cmprehensive and professional' kama ile ya mwaka 2010 iliondokwa na Profesa Kitila tangu chama hicho kilipoanzishwa .

Profesa Kitila Mkumbo alikuwa miongoni mwa viongozi wa Chadema ambao mwaka 2013 walianzisha vuguvugu la kuhoji uhalali wa Mwenyekiti wao kuingiza kipengele cha kuondoa ukomo wa kugombea nafasi ya uenyekiti katika katiba ya Chadema. Vuguvugu hilo lilipelekea kusukwa mkakati wa siri uliowahusisha kina Zitto Kabwe, Samson Mwigamba na Habib Mchange .

Hata hivyo mpango huo kabambe  ulifichuka mapema kabla ya kuanza kwa kamati kuu ya chadema na kujikuta Mbowe akashinda kiubwete uchaguzi na kuwa Mwenyekiti mwaka 2014. Pamoja na kubebeshwa maudhui ya msingi yaliokuwemo kwenye waraka huo, washirika wa Mbowe waliutafsiri na kuuita mkakati wa uasi,  usaliti na hujuma dhidi ya chama.

Japo baadhi ya wanachama na viongozi wachache waliwa sifu na kusema hakuna mwenye haki miliki ya nafasi ya uenyekiti wa chama, Mbowe ameendelea kubaki juu ya kiti chake cha urithi toka kwa watangulizi wake kina Mzee Edwin Mtei na marehemu  Bob Nyange Makani

Katika siasa za vijembe na propaganda, Prof Kitila atakumbukwa kwa kuwapachika jina  wafuasi wa Chadema akiwaita Nyumbu huku akiwalinganisha kitabia na wanyama pori waitwao Nyumbu ambao hutembea, kula, kusafiri na kukaa kwa makundi.

Nyumbu anaaminika ana akili ndogo sana katika kufikiri na kutenda. Profesa Kitila amesisitiza kuwa, Nyumbu hufuata nyayo bila kuhoji, hushangilia akiambiwa ashangilie na hukimbia akiona wa mbele yake anakimbia. Jina Nyumbu limeseelea kutumika tangu enzi hizo katika  siasa za utani na kutupiana matani.

Huenda  Prof Kitila tangu awaite Chadema ni kama kundi la Nyumbu hakuwahi tena kulirudia jina hilo, lakini kauli yake moja ya siku moja ilisambaa mithili ya moto unaowaka nyikani na kuteketeza misitu minene

Kwa sasa Prof Kitila ni Katibu Mkuu  Wizara ya Maji. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Magufuli aliuona uwezo wa Profesa Kitila  akaona ipo  haja ya kumruhusu aitumikie Serikali kwa kumpa nafasi ya juu ya kiutendaji. Kabla ya hapo, kwa miaka mingi Prof Mkumbo alikuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha elimu akiwa amebobea katika masomo ya saikolojia ya elimu.

Ujio wa Prof Kitila Mkumbo katika chama cha mapinduzi haukushtua  sana, maana tayari Watanzania walishaonaiona azma ya wazi ya mwanasiasa huyo msomi kutaka kumsaidia  Rais na Serikali yake ya awamu ya tano.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top