Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwigulu Nchemba ala NondoZzzz

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba jana Novemba 18, 2017 ameweka historia nyingine katika maisha yake baada ya kuhitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Waziri Nchemba amehitimu masomo yake ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika uchumi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nchemba ameweka picha zake na kuandika, anamshukuru Mungu kwamba amehitimu masomo yake ya PhD.

Katika kuandika tasnifu (thesis) yake, Waziri Nchemba aliandika kuhusu“Sterilization of Foreign Exchange Inflows in Tanzania: Extent and Effectiveness.

Katika kuandika tasnifu hiyo, Waziri Nchemba alisimamiwa na wakufunzi, Dr. Jehovaness Aikaeli na Dr. Eliab Luvanda.

Waziri Nchemba amehitimu masomo jana baada ya kutunikiwa shahada hiyo katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City ambapo leo ni kundi la kwanza.

Kundi la pili linatarajiwa kufanya mahafali yao katika ukumbi huo huo, Novemba 21 mwaka huu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top