Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Freemanson adakwa Dar

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Saalaam limemkamata mkazi wa Kinondoni, Rajabu Mohamed (25) maarufu Rajeshi kwa tuhuma za kuwateka wanawake, kuwaingiza kwa nguvu kwenye gari lake, kuwapora na kuwafanyia vitendo vya ukatili huku akijifanya yeye kuwa freemanson.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa akizungumza leo Februari 26, 2018 mbele ya wanahabari, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa eneo la Kinondoni akituhumiwa kuwapata wanawake kwa kuwalaghai kuwa ni mfanyabiashara.

Amesema mtuhumiwa huyo baada ya kuwapora wanawake huzunguka nao katika gari na kuwatishia kuwa ni freemason na anaweza kuwaua kwa kuwanyonya damu au kuwakata maeneo mbalimbali ya miili yao.

 “Kupitia vitisho hivyo wanawake walilazimika kutoa neno la siri la simu zao ambapo alichukua kadi zao za benki na kuwaibia fedha zao kupitia mashine za kutolea fedha (ATM),” amesema Mambosasa.

Amesema mbali na kuwabaka na kuwalawiti huwashusha na kuwatelekeza vichochoroni.

“Hadi sasa tumepokea kesi tatu na nilipomhoji aliniambia kuwa ni kweli alikuwa akifanya vitendo hivyo, lakini kwa sasa ameacha. Hatuwezi kuvumilia vitendo vyake. Upelelezi unaendelea ili kuwabaini wale wote anaoshirikiana nao,” amesema.
Na M - Blog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top