Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Majaliwa : Toka Bilioni 30 mpaka 270 za ununuzi wa dawa nchini


Serikali ya Awamu ya Tano ya Dk. John Mgufuli imeongeza kiwango ununuzi wa dawa katika  vituo vya afya nchini  kutoka shilingi  Biilioni 30 mpaka shilingi Bilioni 270, ambapo katika Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza inapokea milioni mia moja kila mwezi kwa ajili ya manunuzi ya dawa.

 Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu Bw. Kasimu Majaliwa katika Ziara yake Mkoani  Mwanza, ambapo alifungua majengo ya wodi ya akina mama na baba, chumba cha upasuaji,  chumba cha kuhifadhi maiti na chumba cha kujifungulia,  katika kituo cha afya cha Karume kilichopo kata ya Bugogwa ambapo, imegharimu shilingi Milioni mia tano.

Waziri Majaliwa, amewataka wakina mama kupumzika kwenda kupata huduma ya matibabu katika hosptali ya Sekou Toure, kwani wamesogeza huduma hizo karibu yao,  kwenye kituo cha afya cha Karume.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Angeline Mabula, amemuomba waziri Majaliwa kuongeza kwa gali la wagonjwa katika kituo cha afya Karume kwa sasa lipo gali moja la wagonjwa kwani halitoshi kutokana na ongezeko la wagonjwa.

“Nakuomba Mh: Waziri utuongezee gali la wagonjwa kwani lililopo hili moja halitoshi kutokana na ongezeko la wagonjwa kila siku”, alisema Mbunge Mabula.

Baadhi ya wananchi ya Kata ya Bugogwa wameshukuru ujio wa Waziri Mkuu katani hapo kwani, walikuwa wanasumbuka kupata huduma za afya kutokana na uchache wa vifaa tiba, wodi za kisasa pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top