* KANDANDA SAFI LWALILOONYESHA LAWAKUNA WATANZANIA
* KUKUTANA NA APR NUSU FAINALI
Jerry Tegete kulia na Haruna Niyonzima kushoto wakimpongeza Chuji- nyuma nyuma ni Bahanuzi 'Spider Man'. Ushindi wa uhakika jamani raha |
Benchi Yanga likiomba dua wakati Chuji anakwenda kupiga penalti ya mwisho |
Said Bahanuzi 'Spider Man'' aliyeipeleka Yanga robo fainali baada ya kupiga bao mbili pekee katika mechi iliyopita |
Mmanga akiwa kwenye machela baada ya kupoteza fahamu baada ya kuchezea kichapo cha nguvu |
Hapa ni mara
tu baada ya kuanguka akisaidiwa kwa kupepewa na
wenzake
|
YANGA imefuzu kuingia Nusu
Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada
ya kuifunga Mafunzo ya Zanzibar kwa penalti 5-4, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya
dakika 90 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wawakilishi wa Zanzibar
Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ali Othman Mmanga, dakika
ya 34, akiunganisha kona ya Juma Othman Mmanga na Yanga wakasawazisha dakika ya
46, mfungaji Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
Yanga sasa itamenyana na APR
ya Rwanda, keshokutwa ambayo katika Robo Fainali ya kwanza, imeitoa URA ya
Uganda kwa kuifunga 2-1, mabao yake yakifungwa na Jean Claude Iranzi dakika ya
tisa na Suleiman Ndikumana dakika ya 34, wakati la Watoza Ushuru wa Kampala,
lilifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 57.
Katika mchezo huo, Juma Othman
Mmanga alipoteza fahamu na kuwaweka roho juu wachezaji wenzake na mashabiki,
akatolewa nje akipepewa na hakuweza kuendelea na mchezo, lakini taarifa za baada
ya mchezo zilisema anaendelea vizuri.
Kipa wa Yanga Berko aliumia
dakika ya 69 na akatibiwa kwa dakika tatu, kabla ya kutolewa nje dakika ya 72,
nafasi yake ikichukuliwa na Ally Mustafa Barthez ambaye ukaaji wake mazuri
langoni wakati wa penalti ulimfanya Said Mussa Shaaban wa Mafunzo akapiga nje na
kuipa Yanga ushindi.
Saidi Bahanuzi alipiga penalti
ya kwanza, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ya pili, Hamisi Kiiza ya tatu, ya
nne Haruna Niyonzima na Athumani Iddi ‘Chuji’ alipiga ya mwisho na kuwainua
maelfu ya mashabiki wa Yanga Uwanja wa Taifa.
Yanga SC; Yaw
Berko/Ally Mustafa, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin
Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika/Idrissa Assenga, Haruna
Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo/Jerry
Tegete.
Mafunzo; Khalid Mahadhi
Hajji, Ismail Khamis Amour/Hajji Abdi Hassan, Said Mussa Shaaban, Salum Said
Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga/Sadik Habib Rajab, Suleiman Kassim
‘Selembe’, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim/Kheir Salum Kheir
na Ally Juma Hassan.
chanzo: Bin Zubery Blog
Post a Comment