Timu ya Yanga walishinda magoli 2-1 dhidi ya Express, mabao yote yakitiwa kimiani na Jerry Tegete kipindi cha kwanza. Katika kipindi cha kwanza Yanga ilitawala mchezo kwa asilimia 60 dhidi ya Express hata hivyo katika kipindi cha pili mambo yamebadilika ambapo timu ya Express ya Uganda imefanikiwa kupata goli moja la kufutia machozi na kufanya matokeo kubaki hayohayo 2-1.
Kikosi kilichoanza Yanga, kutoka kulia waliosimama Ally Mustafa 'Barthez', Athumani Iddi 'Chuji', Said Bahanuzi, Oscar Joshua, Jerry Tegete na Nizar Khalfan. Walioinama kutoka kulia ni Kelvin Yondan, Nadir Cannavaro, Juma Abdul, Frank Damayo na Simon Msuva.
Chanzo: Bongostars blogspot
Post a Comment