Kiongozi wa Madaktari nchini Dk. Steven Ulimboka amesafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu zaidi yaliyotokana na kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa vibaya baada ya kufanya unyama huo na watu wasiojulikana. Mahali alipopelekwa Dk. Ulimboka kwa ajili ya matibabu imebakia kuwa ni siri kubwa huku wapo wanaosema amepelekwa India, wengineo wakisema amepelekwa Afrika Kusini lakini baadhi ya wataalamu wa afya wamesema amepelekwa nchini Kenya. Hakuna uthibitisho sahihi wa mahali alipokwenda.
Dk. Ulimboka anaondoka nchini huku akiacha matukio
matano ya ajabu na ya kushangaza zaidi hapa nchini. Matukio hayo ni kama
ambavyo amekuwa akiyasimulia pindi alipokuwa akihojiwa na Waaandishi wa habari.
Matukio hayo ni kama vile;-
1. Dk.
Ulimboka alitekwa, kupigwa na kuumizwa zaidi ambapo kwa mateso aliyoyapata ni
dhahiri waliofanya kitendo kile walikuwa na lengo la kukatisha uhai wake. Jambo
la kushangaza ni kwa watu wale ambao Dk. Ulimboka anadai walikuwa na silaha za
moto lakini walishindwa kumfyatulia hata risasi moja. Hakika, Mwenyezi Mungu yu
pamoja na Dk. Ulimboka.
2. Licha
ya kupewa mateso ya ajabu na hata kufungwa kamba mikononi na miguuni huku akiwa
hoi bin taabani kwa kipigo lakini aliweza kujiburuza kutoka ndani ya msitu wa
Mabwepande mpaka kufika pembezoni mwa msitu ambapo aliokolewa na msamaria
mwema aliyekuwa anapita.
3. Uchunguzi
wa jopo la Madaktari kupitia vipimo walivyomfanyia wamegundua athari mojawapo
ambayo Dk. Ulimboka ameipata ni mtikisiko wa Ubongo. Lakini ajabu ya firauni ni
kuwa Dk. Ulimboka bado ana kumbukumbu nzuri na mambo yote aliyofanyiwa
anayakumbuka vyema na utibitisho wa hilo ni namna anavyosimulia mkasa wake
mzima jinsi ulivyokuwa. Huyo ni Mungu tu wa Meshack, Daniel, na Abednego.
4. Dk
Ulimboka anamfahamu kila mmoja anayekwenda kumuona mpaka na utani wanaotaniana
(kama upo lakini) licha ya kuwa amepatwa na mtikisiko wa Ubongo.
5. Licha
ya kwamba alikuwa I.C.U lakini inavyosemekana mmojawapo wa Afisa aliyemtembelea
aliweza kukumbukwa vyema na Dk. Ulimboka alimwambia amrudishie wallet (poshi ya
kuhifadhia pesa) yake, funguo zake za gari pamoja na Document zake. Inavyosemekana
yule Bwana alitoka mbio maeneo yale kimya kimya.
Watanzania tuendelee kumwombea Dk. Steven Ulimboka
apone kwa haraka kwani uwepo wake ni muhimu sana kwa upiganiaji haki kwa wana
wa huduma za kiafya na ni muhimu sana kwa mustakabali wa mapambano ya adui “maradhi”
kwa Watanzania wote wa Taifa hili kwani Madaktari wakitutibu pasipo simanzi,
afya zetu zitaimarika pia.
Post a Comment