|
Askari
wa vikosi vya Ulinzi na Usalama wakiwa wamebeba moja ya miili ya watu
waliopoteza maisha katika ajali ya boti ta Stargic iliyotokea jana
karibu kabisa na Unguja.Picha na Ramadhan Othman
*BOTI YAZAMA NA ABIRIA 250, KATI YAO 60 WAHOFIWA KUFARIKI DUNIA Waandishi Wetu WATU
60 wanahofiwa kufa maji na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya boti
iliyokuwa imebeba abiria wanaokadiriwa kufikia 250 ikitokea Dar es
Salaam kwenda Unguja, Zanzibar kuzama baharini.Hii ni ajali ya pili
mbaya kutokea katika kipindi cha miezi 10 tangu ilipotokea nyingine ya
Meli ya Mv Spice Islander ambayo inakadiriwa kuwa watu wapatao 200
walifariki dunia.Boti hiyo iliyoondoka jana Dar es Salaam majira ya saa
6:00 mchana na kutarajiwa kufika Bandari ya Malindi, Zanzibar saa 9:30
jioni, ilizama eneo la Pungume karibu kilomita 48 kutoka Bandari ya
Zanzibar. Inaelezwa kuwa, ilianza kuzama saa 7:30 mchana kutokana na kupigwa na mawimbi mazito ya bahari.
Hata
hivyo, Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Hamad Masoud
Hamad alithibitisha vifo vya watu 12 hadi vilivyoripotiwa ilipotimu saa
12:30 jioni jana wakati kazi ya uokoaji ikiwa inaendelea.
Baadaye
saa 1:00 Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara hiyo, Nafisa Madai
aliwaambia waandishi wa habari kuwa idadi hiyo ilikuwa imeongezeka hadi
kufikia 24 na majeruhi walikuwa 145.Madai alisema wakati boti hiyo
inaondoka Dar es Salaam, ilikuwa na abiria 250 wakiwamo watoto 31 na
wafanyakazi tisa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar, Said Shaaban akizungumzia ajali ya boti hiyo ya Mv
Skad, inayomilikiwa na Kampuni ya Meli Seagull alisema: “Vikosi vya
uokoaji tayari vinaelekea katika eneo hilo ili kusaidia majeruhi na
kufuatilia yaliyotokea.”
Maofisa kadhaa wa Serikali wakiongozwa
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi walifika
Bandari ya Malindi na Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar,
Hamad Masoud Hamad aliongoza msafara wa viongozi wengine kwenda katika
eneo la tukio.
Awali, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi alisema kuwa, hadi alipopata taarifa, watu waliokuwa
wamefariki dunia ni saba na 124 ndiyo waliokuwa wameokolewa. Alisema
meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 300 na waliosafiri siku ya tukio
hawazidi 250.
Awali, taarifa zilieleza kuwa watu 10 waliokolewa
na maiti zaidi ya 60 zimenasa katika boti hiyo na kuvifanya vikosi vya
uokoaji vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi na KMKM kupata
wakati mgumu kwenye zoezi la uokoaji.Kazi ya kuokoa maisha ya watu
waliozama kwenye boti hiyo na kuopoa maiti ilifanywa kwa kutumia boti
nne zikiwamo za Serikali na zile zinazomilikiwa na Kampuni ya Azam
Marine.Hata hivyo, ilielezwa kwamba boti za polisi zilichelewa kwenda katika eneo la tukio kutokana na kukosekana kwa mafuta. Akizungumza
na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufika bandarini, Balozi
Seif aliwataka wananchi kutulia na kusubiri wakiwa nyumbani wakati
Serikali ikifanya juhudi za uokoaji.
Shughuli nyingi za usafiri
zilivurugika kutokana na tukio hilo na Meli ya Mv Sea Bus ililazimika
kufuta safari zake kupisha kazi hiyo ya uokoaji. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imesema inafuatilia tukio hilo kwa karibu ili kubaini chanzo. Ofisa
Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alisema jana muda mfupi baada ya
ajali hiyo kuwa, wanawasiliana na Kituo cha Utafutaji na Uokoaji Majini
(MRCC), ili kupata taarifa kamili kabla ya kuujulisha umma. Spika Makinda achafua hali ya hewa.
chanzo: Mwananchi |
on Thursday, July 19, 2012
Post a Comment