Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SUMATRA: MELI YA MV SKAGIT ILIKUWA NA ABIRIA 248, WATOTO 31 NA MABAHARIA 9


MAMLAKA ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na maji (SUMATRA),imesema meli ya MV Skagit iliyopata ajali visiwani Zanzibar, iliondoka Bandari ya Dar es Salaam saa 06.05 mchana juzi ikiwa na abiria 248, watoto 31 pamoja na mabaharia 9.

Meli hiyo inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul Transport, ilipata usajili katika Mamlaka ya usafiri  Bandari Zanzibar (ZMA)ikiwa na uzito wa meli (GRT)96.

 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Meneja Mawasiliano David Mziray, alichanganua kuwa cheti cha ubora wa meli hiyo kilitolewa Agosti mwaka jana na kumalizika mwezi huo mwaka huu.

“Mv Skagit ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 pamoja na mizigo tani 26,  hivyo kulingana na idadi ya abiria 288 walioondoka katika chombo hicho isingeweza kuleta madhara kama hayo, ila tunawasiwasi waliongeza abiria njiani au mawasiliano ya hali ya hewa” Kwa mujibu wa Mziray.

Aidha, anafafanua kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha hadi sasa ni zaidi ya 34, majeruhi 146 wakati wengine wakiendelea kutafutwa.

“Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kwa msaada wa Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro 111, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar 1, Polisi wa majini, pamoja na Navy, hata hivyo bado taarifa sahihi za waliopoteza maisha hazijapatikana kulingana na watu hao kuokolewa katika mazingira tofauti” alibainisha Mziray.

Hata hivyo alisema baadhi ya viongozi wa Sumatra wamekwenda katika tukio hilo kwa ajili ya kushirikiana na ZMA ili kuokoa maisha ya watu hao.
 
chanzo: Fullshangweblog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top