Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Jukwaa la Mabunge ya nchi za SADC kuunda Bunge lake

Na Prosper Minja-Bunge
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (Mb) yuko Maputo Msumbiji kuhudhudhuria mkutano wa 31 wa Jukwaa la Mabunge ya nchi wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusinin mwa Afrika- SADC-PF. Mkutano huo ulionza leo tarehe 11 Julai 2012 utajadili pamoja na mambo mengine uwezekano wa kuunda Bunge la SADC. Jambo lingine linalojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na kuimarisha demokrasia katika chaguzi mbalimbali za nchi wanachama.
Tayari chombo hiki (SADC-PF) kimeanzisha utaratibu wa kusimamia chaguzi mablimbali na kutoa taarifa iwapo katika chaguzi hizo kumekuwa na ukiukwaji wa sheria na taratibu za uchaguzi.
Katika mkutano huo Tanzania imepwa jukumu la kujifunza muundo na uendeshaji wa Bunge la Afrika Mashariki. Wakati huo huo Afrika Kusini imepwa jukumu la kujifunza muundo na utendaji wa Bunge la Umoja wa Ulaya. Nchi hizi mbili zitawasilisha taarifa kwenye kikao cha SADC-PF kitakachofuata ili kuona ni kwa jinsi gani Bunge hilo litakavyoweza kuundwa.
SADC-PF imekuwa mstari wa mbele kutoa misaada na kuelimisha umma kuhusu virusi na kuishi na virusi vya UKIMWI na kujikinga na maambukizi mapya UKIMWI. Aidha chombo hiki kimeshatoa mwongozo wa kisheria kuhusu UKIMWI na jinsi ya kuuhamasisha umma.
Katika Mkutano huo Spika Makinda naongoza ujumbe wa wajumbe watano ambao ni: Mhe. Stella Manyanya, Mhe. Anna Abdallah, Mhe. Habib Mnyaa, Mhe. Titus Kamani na Kaimu Katibu wa Bunge Bwana Jossey Mwakasyuka.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top