Waandishi wa mitandao ya kijamii na tovuti kupewa tuzo kutokana na
jitihada na mafanikio yao.
Tuzo hizo kuitwa “ Tuzo za umahiri wa digitali za
Vodacom”
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa
waandishi bora kumi mahiri katika mitandao ya kijamii kutokana na umahiri
wao.
Tuzo hizo ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za
Vodacom”, zitatolewa kwa washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao
ikiwa ni kwa mala ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya
Vodacom.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema
kuwa Waandishi wa mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa taarifa
mbalimbali ndani ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa.
Wapo waandishi wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala
mbalimbali kuhusu biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja, Ni kwa
sababu hii ndio maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana na mabadiliko
waliochangia katika utoaji wa taarifa” Alisema Meza.
Baadhi ya
sifa ambazo zitapewa kipaumbele katika tuzo hizi, pamoja na mambo mengine, ni
ubunifu na utoaji wa taarifa za kijamii, Kuzingatia ueledi wa uandishi na uhuru
wa vyombo vya habari, mahusiano na wasomaji katika utoaji wa taarifa, umahiri wa
picha na ushirikishwaji wa vyombo vingingine.
Waandishi wa
mitandao ya kijamii wata shindanishwa kadri inavyowezekana ili kuwawezesha
kuongeza ueledi na umahiri katika kazi zao.
Kampuni ya
Vodacom Tanzania pia itaanzisha mfuko wa fedha wa maendeleo ya digitali, Kwa
mujibu wa Meza fedha hizi zitatumika katika kuendeleza umahiri na kuboresha kazi
katika mitandao ya kijamii na tovuti.“Huu ni mchango kutoka Mfuko wa M-pesa
ambapo waombaji wataweza kuzitumia katika udhamini na kuendeleza shughuli zao”,
Alisema Meza na kuongeza kuwa, “ Tunathamini mchango wa kila mtu, na tunahitaji
waandishi wa mitandao ya kijamii wote waendelee kufanya kazi zao nasi
tutaendelea kuthamini na kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”
Post a Comment