VITA ya
kuwania kiatu cha dhahabu cha Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame imezidi kupambana moto, baada ya John Raphael Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC
na Hamisi Kiiza ‘Diego’ wa Yanga kutimiza mabao matano kila mmoja, hivyo
kulingana na Said Bahanuzi ‘Spider Man’ anayeshika nafasi ya pili, nyuma ya
Taddy Etikiama na AS Vita ya DRC, mwenye mabao sita.
Wachezaji
wote hao wanne, watakuwa na fursa ya kuongeza mabao yao Jumamosi, Bocco, Kiiza
na Bahanuzi wakicheza fainali kati ya Yanga na Azam, wakati Taddy akiiongoza AS
Vita katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, dhidi ya APR ya Rwanda.
Wengine
waliomo kwenye kinyang’aniyo hicho ni Suleiman Ndikumana wa APR mwenye mabao
mabao matatu, ambaye pia anaweza kuongeza mabao yake katika mchezo wa kusaka
mshindi wa tatu keso.
Abdallah
Juma ‘Dullah Mabao’ wa Simba SC timu yake imetolewa akiwa ana mabao mawili sawa
na Leonel St Preus wa APR, Didier Kavumbagu wa Atletico, Feni Ali na Robert
Ssentongo wa URA.
WANAOONGOZA
KWA MABAO:
Taddy
Etikiama AS Vita 6
Said
Bahanuzi Yanga SC 5
Hamisi Kiiza
Yanga SC 5
John Bocco
Azam FC 5
Suleiman
Ndikumana APR 3
Abdallah
Juma Simba SC 2
Leonel St
Preus APR 2
Didier
Kavumbagu Atletico 2
Feni Ali
URA 2
Robert
Ssentongo URA 2
Chanzo: Bongostaz
Post a Comment