Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAWAZIRI WAKUU WATOA ANGALIZO VITAMBULISHO VYA TAIFA



MAWAZIRI wakuu wastaafu wameonya uandikishaji wa vitambulisho vya taifa unaoendelea nchini, chini ya uratibu na Mamlaka ya Vitambulisho hivyo nchini (NIDA) kuendeshwa kwa uzalendo na kamwe kutoruhusu wasio raia kuandikishwa kwani vinaweza kutumika vibaya siku zijazo.

Mawaziri hao ambao ni Edward Lowassa, Frederick Sumaye, John Malecela, Jaji Joseph Warioba, Salim Ahmed Salim na Cleopa Msuya walitoa rai hiyo juzi usiku wakati wakizungumza katika mwendelezo wa vipindi maalumu kuhusu uandikishaji huo wa vitambusho vya taifa unaoendelea nchi ambacho kilirushwa hewani na Channel 10.


“Eneo moja ambalo lazima tujiadhari nalo sana ni eneo la nani amepewa kitambusho. Kuna rafiki yangu mmoja anatoka mikoa ile ya Kigoma na Rukwa ananiambia siku hizi inawezekana kabisa kwa waliokuwa wakimbizi ambao wamehamia maeneo yale wakamchagua mbunge au diwani kwa sababu wamekuwa wengi.

“Sasa ni vema wale ambao tumekubali wawe raia wa nchi yetu vema... Mimi hofu yangu ni wasio raia ambao bado wako mipakani, lazima tuwe makini mtu akipata uraia wa Kitanzania awe kweli ni Mtanzania,” alisema Lowassa.


Naye Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, Frederick Sumaye, alisema uzalendo unahitajika katika suala hilo na kamwe jamii isibeze na kulipuuza zoezi hilo kwa kusema ni mradi mwingine wa serikali bali kujitoa kulifanikisha kwa manufaa ya Watanzania kwa jamii iliyopo, watoto na vizazi vijavyo.
Alionya kwamba kosa lolote litakalojitokeza wakati wa mradi huu litaigharimu nchi mbele ya safari, hivyo unatakiwa kutofanyika kwa makosa.


Naye John Malecela alisema suala la uzalendo litatokana na serikali za vijiji na ndio maana wakati huo iliamuliwa kwamba serikali ya kijiji iwe na watu 25 ambao watakuwa watawala wa eneo hilo na jingine ni mipaka.







Naye Jaji Mstaafu, Joseph Warioba, alisema wananchi hawana budi kufahamu kwamba zoezi hilo ni kwa manufaa yao lakini pia ni kazi ya vyama vya siasa na viongozi wengine kufanya jitihada kuelimisha wananchi kufahamu kuhusu umuhimu wa vitambulisho.

Chanzo: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top