Mlima Kilimanjaro unavyooekana ukiwa umezungukwa na uoto wa asili wa misitu huku ukipambwa na Wanyama wa kuvutia
Mlima Kilimanjaro unavyooneka ukiwa angani umezungukwa na theruji ya barafu
Na
Emmanuel J. Shilatu
Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika, pia ni wa
pili kwa urefu Duniani. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa
Kilimanjaro. Una urefu wa futi 19,340 (mita 5,895). Hali halisi Kilimanjaro ni
zaidi kuliko mlima tu ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na
Shira. Hii mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja hivyo si vibaya
kusema Kilimanjaro ni mlima.
Mlima huu ambao ni mrefu kuliko yote katika Bara la Afrika
na wenye barafu katika kilelele chake ingawa, upo kwenye eneo la joto karibu na
Mstari wa Ikweta. Mathalani, Kibo ina theluji na barafuto kadhaa ndogo
Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha
Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko takriban
mnamo mwaka 1730.
Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru Peak. Mtu wa kwanza
wa kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu
aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller mnamo tarehe 6
Oktoba, 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu
"Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kijer.:Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa
heshima ya Kaisari wa Ujerumani.
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani kutokana na
mandhari nzuri ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote Afrika na
inapatikana katika nchi ya Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za
mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini. Kilele cha Kibo
chenye urefu wa mita 5895 (futi 19340) ndio kivutio kikubwa kwa wageni kutoka
ndani na nje ya nchi kutokana na kufunikwa na theruji.
Mlima huu ni moja kati ya milima ambayo kilele chake
hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka
kila pande za dunia.
Safari ya kupanda mlima huu humpitisha mpandaji katika kanda
za hali ya hewa tofauti kuanzia ile ya nchi za tropiti hadi arktiki.
Zaidi ya watalii 20,000 hupanda mlima huu kila mwaka
wakiwemo wageni kutoka nje ya nchi na Watanzania. Mpandaji wa mlima huu
huhitaji angalau siku tano, siku tatu kupanda na siku mbili kuteremka.
Kuna njia sita ya kupanda mlima Kilimanjaro hadi kileleni. Njia
iliyo rahisi na maarufu zaidi ni ile ya kuanzia lango la Marangu, ambako ndiyo
makao makuu ya hifadhi.
Wanyama kadhaa hupatikana katika msitu unaozunguka Mlima
Kilimanjaro wakiwemo mbega, nyani, nyati, chui, tembo, swala na ndege.
Ndugu zangu Watanzania, Ukiwa katika mandhari ya Mlima
Kilimanjaro sio tu utaona mlima bali pia utapata fursa ya kujihisi upo mbugani
kutokana na uwepo wa Wanyama wanaozunguka hifadhi hiyo. Kama haitoshi kwenye
Mlima Kilimanjaro ni sehemu pekee (kwa Tanzania nzima) utakayoweza kuona Barafu
mithili ya theruji nyeupe. Karibuni tuutembelee Mlima Kilimanjaro ili tujionee
fahari ya kipekee Tanzania na Barani Afrika.
Post a Comment