Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SABASABA IMETOA SOMO LA KILIMO MJINI

Msimu wa sabasaba kwa mwaka huu 2012 umekwisha ambapo nilipata wasaa wa kutembelea maonyesho hayo. Yapo mambo mengi sana yaliyonivutia ila kubwa ilikuwa ni somo la mfano wa namna gani hata watu wa mjini wanaweza wakadumisha kilimo kwanza. Katika hilo nilishuhudia mazao kama bamia. spinach, matango, mahindi yakiwa yamestawi mno kwa utaribu wa upandaji wa Sentimeta 60 (kwa nyuma ama mbele ya zao) na sentimeta 90 (kushoto ama kulia kwa zao jingine). Hakika yalikuwa yamestawi mno.
Mfano wa upandaji wa Bamia kwa waishio mijini na ikaweza kustawi mno
Blanka Ngowi akishangaa namna ambavyo Spinach zilivyostawi ndani ya viwanja vya sabasaba. 
Haya na matango yakiwa yamepandwa kwa mtindo wa kwenda juu kwa vipimo vya cm 60 kwa cm 90

Kama haitoshi walituonyesha namna gani ya kuyamwagilia mpaka yastawi tena kwa njia rahisi ya kutumia pampu ya mkono isiyotumia mafuta, jua wala gesi ambapo watu wengi walishangaa mno kama ambavyo Blanka Ngowi akiwa ameduwaa. Mbegu pamoja na hiyo pampu zinapatika kwa bei nafuu sana.

Ndugu zangu, tusiishie kusema maisha magumu wakati hatujushulishi. Maisha ni marahisi sana kama ukijituma, na ni magumu mno endapo utakuwa goigoi. Kupanga ni kuchagua, kazi kwako.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top