Katibu Mkuu UVCCM ,Mh.Shigela Martin
akihutubia wananchi wa Mtwara
Tambwe Hiza wa CCM Makao Makuu akihutubia wananchi masuala muhimu ya kujenga nchi na yenye kuleta maendeleo kwa Taifa |
Katibu mkuu wa umoja wa vijana wa CCM Martin Shigela amewataka
wananchi wa mkoa wa Mtwara kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao wakati Tume ya
kuratibu maoni ya katiba mpya itakapofika mkoani humo kukusanya maoni ya
wananchi,amesema CCM haina agenda yoyote iliyojificha katika upatikanaji wa
katiba mpya itakayotokana na utashi wa
wananchi wenyewe.
Alitilia mkazo kwa
wananchi kutoa maoni yao kwa amani bila kuingilia uhuru wa
wengine,aliwaasa kuangalia mambo ya muhimu ambayo wanaona yatasaidia kuiweka
nchi katika amani na kuendelea kutoa fursa ya maendeleo kwa wananchi kama ilivyo
sasa.
Kuhusu mgombea binafsi alisema CCM haipingi kama wapinzani wanavyotangaza
na kama wananchi wanalitaka hilo katika kukuza demokrasia nchini waliseme na
litatekelezwa bila wasi wasi na kwamba CCM ndiyo itafaidika zaidi kwa kuwa
wanachama wake hawataenda upinzani kutafuta nafasi za kugombea kama ilivyo sasa
ambapo wanakwenda huko huku wakiamini vyama hivyo havina sera yoyote ya
maendeleo ya Taifa zaidi ya kutaka
utawala.
Pia alielezea fursa mbali mbali za mkoa huo zilizoletwa na serikali ya CCM
na zitakazoendelea kuletwa katika kipindi kifupi kijacho.
Kabla ya hapo mjumbe
aliefuatana naye katika msafara wake Tambwe Hiza alizungumzia hali ya nchi
iloivyokwenda mbele kimaendeleo tangu tulipopata uhuru ikiwa nin pamoja na
uanzishaji wa shule nyingi za msingi karibu na maeneo wanayoishi wananchi
kinyume na hali ilivyokuwa kabla ya kujitawala na miaka ya mwanzo ya uhuru
ambapo kila Tarafa ilikuwa na shule moja ya msingi jambo lililopelekea watoto
kutembea umbali mkubwa kwenda shule.
Halikadhalika aliwabeza wanaodai miaka 50 kuwa
hakijafanyika kitu kwa kutoa mifano ya ya vyuo vikuu vilivyoanzishwa baada ya
uhuru ambavyo havikuwepo kabla idadi ya wanafunzi wanaoingia sekondari hivi sasa
akitolea mfano wa idadi ya watoto 5 kati ya watoto 100 waliofaulu waliokuwa
wakienda sekondari wakati wa serikali ya awamu ya kwanza kwa kuwa wakoloni
hawakujenga za kutosha,wanafunzi waliongezeka kufikia 13 wakati wa awamu ya
pili,21 awamu ya tatu na awamu hii ya Rais Kikwete imefikisha 97 kati ya mia
huku baadhi ya mikoa ikifikia 100/100
chanzo: CCMBlog
Post a Comment