Ngorongoro wakitoka uwanjani vichwa chini |
Na Bongostaz
TIMU ya soka
ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo imeanza
vibaya kampeni za kuwania kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo,
zitakazofanyika nchini Algeria mwakani, baada ya kufungwa na Nigeria mabao 2-1,
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Achaji Gero; Aliyefunga mabao yote ya Nigeria |
Hadi
mapumziko, Nigeria, Flying Eagles walioonekana kutumia wachezaji waliozidi umri,
walikuwa mbele kwa mbele kwa mabao 2-0 katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya
pili, yote yakitiwa kimiani na mshambuliaji wa Enugu Rangers, Achaji Gero katika
dakika ya pili na 44.
Kipindi cha
pili, Ngorongoro walibadilika na kucheza vizuri, wakiwazidi wapinzani wao
kumiliki mpira na kasi ya mchezo na hatimaye wakafanikiwa kupata bao la kufutia
machozi, lililofungwa na Atupele Green dakika ya 50, akimalizia krosi ya
Ramadhani Singano ‘Messi’.
Ngorongoro
wangeweza kupata mabao zaidi, kama wangecheza soka ya chini, lakini kutia krosi
za juu kwenye lango la Nigeria ilikuwa ni kuwatesa washambuliaji wao wafupi,
Atupele na Simon Msuva.
Kwa matokeo
hayo sasa, Ngorongoro wanahitaji ushindi wa angalau wa mabao 2-0 katika mchezo
wa marudiano Nigeria wiki mbili zijazo, ili kusonga mbele.
Baada ya
mchezo huo, kocha wa Ngorongoro Heroes, Mdenmark Jakob Michelsen alisema kwamba
ataongeza nguvu katika kikosi chake kwa kuwaita wachezaji wawili wanaocheza nje,
kiungo Adam Nditi wa Chelsea na Thomas Ulimwengu wa Tout Puissant Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), sambamba na nyota wengine waliokwenda
Ujerumani n TSU kwenye michuano ya Fallerhof.
Huu unakuwa mchezo wa tatu mfululizo Ngorongoro inafungwa nyumbani tangu Michelsen apewe timu hiyo akirithi mikoba ya Kim Poulsen, ambaye amepandishwa timu ya wakubwa, Taifa Stars.
Awali, Ngorongoro walifungwa mechi mbili za kirafiki na Rwanda mwezi huu, moja Chamazi 2-0 na nyingine Taifa, 2-1.
Huu unakuwa mchezo wa tatu mfululizo Ngorongoro inafungwa nyumbani tangu Michelsen apewe timu hiyo akirithi mikoba ya Kim Poulsen, ambaye amepandishwa timu ya wakubwa, Taifa Stars.
Awali, Ngorongoro walifungwa mechi mbili za kirafiki na Rwanda mwezi huu, moja Chamazi 2-0 na nyingine Taifa, 2-1.
Katika
mchezo, kikosi cha Ngorongoro kilikuwa; Barwany Khomein, Omega Seme, Jamal
Mroki, Issa Rashid, Ruhana Samir, Yarouk Ramadhan, Kheri Salum/Jerome Lambele,
Frank Damayo, Simon Msuva, Atupele Green na Ramadhan Singano.
Flying
Eagles; Samuel Okani, Hassan Abubakar, Ahiyu Mohamed, Ikechukwu Okine, Chizoba
Amaefule, Agboyi Oubokha, Moses Orkuma, Chidi Osochukwu, Yahaya Adam/Harrison
Egbune, Achaji Gero na Aminu Omar/Uchw Agbo.
Post a Comment