Mbunge,
mshambuliaji wa Yanga, akiwatoka mabeki wa Simba, wakati wa mchezo wa kirafiki
wa Wabunge mashabiki wa Yanga na Wabunge mashabiki wa Simba, uliochezwa leo
jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Wabunge hao walitoka sare ya
bila kufungana katika dakika 90 za mchezo na mwamuzi wa mchezo huo Othman Kazi,
akaamuru timu hizo kupigiana penati, ambapo Simba wameweza kuibuka kidedea kwa
penati 3 kwa 2.
Mhe.
Majaliwa, akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa 'Yanga'.
Mshambuliaji
wa Yanga, akiwatoka mabeki wa Simba.
Kocha
mpya wa Yanga, akiwa katika Benchi la wachezaji wabunge wa Yanga, wakati wa
mchezo huo, pamoja na waheshimiwa wabunge wa Benchi la ufundi.
Wachezaji
wabunge wa akiba wa Yanga katika benchi lao.
Wachezaji
wa akiba wabunge wa Simba wakiwa katika benchi lao. Vipi Mh. Zito umelala ama upo bize na BBM?
Sehemu
ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Mara
wachezaji walianza kuanguka kwa kukamatwa na misuri, hapa ni Nahodha wa Simba,
Amos Makala, akisaidiwa na beki wake, William Ngeleja.
Mshambuliaji
wa timu ya Wabunge wa Simba, Zitto Kabwe (kushoto), akichuana na beki wa timu ya
Wabunge wa Yanga, Michael Kadebe katika mchezo wa kuchangia fedha kwa ajili ya
ujenzi wa mabweni ya wanafunzi vijijini.
Mshambuliaji wa timu ya Wabunge wa Simba, Zitto
Kabwe akimtoka beki wa Wabunge wa Yanga, Abdallah Haji.
Kipa
wa Simba, Joshua Nassari, akijaribu kuifuata penati bila
mafanikio.
Mchezaji
wa Simba, akishangilia baada ya kupiga penati ya mwisho iliyowahakikishia
ushindi.
'Raha
ya Ushindi kicheko', Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, akicheka cheko la furaha
baada ya kibuka washindi katika mtanange huo.
Wachezaji wa Simba (Wabunge)
wakishangilia ushindi kwa mtindo wa kucheza kwaito baada ya kuwafunga watani wao wa Yanga (Wabunge) kwa
penalti 3-2.
Pole sana Mheshimiwa, huo ndio mpira
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam katika mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga
(Wabunge) wakati wa TAMASHA LA MATUMAINI ambapo wabunge wapenzi wa timu ya Simba
wameibuka kidedea kwa penalti 3-2. Simba wamefunga penalti 3 wakati Yanga
wakifunga 2.
(PICHA NA GPL NA SUFIANI MAFOTO)
Post a Comment