Huku Wabunge wa CCM wakiwa wamekaa, Wabunge wa Chadema waliamua kutoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akianza hotuba yake ya
kulifungua rasmi Bunge la 10 kwa madai ya kuwa hawamtambui. Tukio hilo lilitokea mnamo Novemba 18, 2010
tukio la Julai 28, 2011 liliwahusisha Godbless Lema
wa Arusha Mjini (ambaye Ubunge wake ulithibishwa na Mahakama haukuwa halali),
Tundu Lissu wa Singida Mashariki na Mchungaji Peter Msigwa wa Iringa Mjini
walitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Job Ndugai.
Walitolewa muda mfupi baada ya Lema (aliyekuwa
Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi), kumaliza kusoma hotuba yake.
Baada ya Lema kumaliza kuwasilisha hotuba yake,
Lukuvi alisimama akiomba kutoa taarifa na pia mwongozo wa Naibu Spika kutokana
na hotuba ya Lema kujaa maneno ya uchochezi na yasiyo ya kistaarabu.
Wakati Lukuvi akiendelea kuzungumza, Lema, Lissu na
Msigwa kwa nyakati hiyo hiyo nao pia
walitaka kumkatisha Lukuvi ili wao wazungumze lakini Naibu Spika aliwaambia
wakae na wazime vipaza sauti vyao, hawakumsikiliza bali waliendelea kuligeuza
Bunge kuwa gulio kutoka kuwa mhimili wa dola.
Waliendeleza jeuri yao ya kuvunja sharia hali
iliyomlazimu kuchukua hatua ya kuwatoa nje ya Bunge kwa kukiuka kanuni ya Bunge
kwa kuzungumza bila ruhusa.
Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa
nje ya ukumbi wa Bunge na Askari Polisi wa
Bunge.
Hiyo ilitokea mnamo Julai 27, 2011 ambapo Mbunge wa
Nyamagana, Ezekiel Wenje aliyeomba mwongozo wa Spika kutumia kanuni ya 11 kwa
kudai kamati ya uongozi ya Bunge ilifanya uamuzi kinyume na kanuni za Bunge na
kukiita kitendo hicho ni “dark market”.
Neno hilo lilimfanya Spika kuchefuka na lugha za
maudhi Bungeni zilizo kinyume na kanuni za Bunge na akaamulu atolewe nje. Wenje
alijikaanga mwenyewe si kwa kukosea utaratibu wa kuomba mwongozo bali ni kwa
kutoa lugha ya maudhi Bungeni.
Mnamo Juni 15, 2012, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika
aliendeleza utovu wa nidhamu dhidi ya kanuni za Bunge kwa kutoa lugha ya maudhi
na za kejeli ambapo Ndugai alitumia kanuni ya 73 (2) na kumtoa nje ya ukumbi wa
Bunge kama anavyoonekana pichani akisindikizwa na Maaskari
Post a Comment