Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANANCHI WAHIMIZWA KUSHIRIKI KUWAKUMBUKA MASHUJAA

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati) akiongea na waandishi wa habari Katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es Salaam kueleza namna mkoa ulivyojipanga kufanikisha sherehe za maadhimisho ya siku ya mashujaa itakayofanyika kitaifa tarehe 25, Julai 2012 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
 
Askari Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watakaoshiriki kwenye gwaride wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa wakiendelea na mazoezi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Kiongozi wa mabalozi wan chi za Afrika wanaoishi nchini Tanzania Balozi Ibrahim Mukubi kutoka Uganda akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe ya siku ya mashujaa itakayofanyika tarehe 25, Julai 2012.


Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es salaam.
Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja tarehe 25 Julai 2012 jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam , Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na kufafanua kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Amesema katika maadhimisho hayo kwa upande wa mkoa wa Dar es salaam baadhi ya barabara zitafungwa ikiwemo barabara ya Nyerere, Uhuru na Bibi Titi Mohamed ili kuhakikisha usalama kwa wale wote watakaohudhuria maadhimisho hayo na kuongeza kuwa katika kuboresha maadhimisho hayo kamati ya maadhimisho itaweka luninga katika maeneo yote muhimu ili kuwawezesha wananchi kuona yanayotendeka wakati wa maadhimisho hayo.
Aidha Bw. Meck Sadiki amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbukumbu muhimu katika historia ya Tanzania kwa kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa na kuilinda Tanzania.
“ Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu sana katika historia ya nchi yetu kwani tunawaenzi mashujaa wetu waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa, kuilinda na kudumisha amani na utulivu wan chi yetu”
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top