Santi Cazorla
Nuri Sahin
Arsenal
inajitahidi kukamilisha utiaji saini wa makubaliano ya mkataba wa
kudumu na mchezaji Santi Cazorla kutoka klabu ya Malaga pamoja na mcheza
kiungo mwenzake Nuri Sahin anayeingia kwa makubalino ya mkopo kutoka
klabu ya Real Madrid.
Mpango
wa kuhama kwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uhispania Cazorla mwenye
umri wa miaka 27 kumekua na utata wa shida ya fedha inayoikumba klabu ya
Malaga hata hivyo anatazamiwa kupitia utaratibu wa afya wiki hii.
Mcheza
kiungo wa timu ya Taifa ya Uturuki mwenye umri wa miaka 23 Nuri Sahin
atajiunga na Arsenal chini ya mpango wa mkopo wa mwaka mmoja na Real
Madrid.
Lililobaki
ni baina ya mchezaji Sahin kukubaliana na klabu ya Arsenal juu ya
malipo na marupurupu. Kuna uwezekano mkubwa kwa wachezaji hawa
kuhitimisha utaratibu huu kabla ya msimu mpya kuanza.Bado Sahin
hajapangiwa siku ya kufanyiwa majaribio ya afya. Arsenal inaanza msimu
mpya kwa pambano la ugenini dhidi ya Sunderland mnamo tareh 18 Agosti.
Tayari
Gunners imewasajili wachezaji wawili mshambuliaji Lukas Podolski kutoka
klabu ya Cologne na mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud aliyekuwa
akichezea klabu ya Montpellier.
Pamoja
na hayo yote wingu zito bado limegubika majaliwa ya nahodha Robin van
Persie, ambaye ametamka kua hatoongezea mkataba wake unaomazika mwaka
2013.
Usajili
wa wacheza kiungo Cazorla pamoja na Sahin ingawa hakuna uhusiano na
mizengwe ya Van Persie lakini umechagizwa na habari kwamba mcheza kiungo
wa Arsenal Jack Wilshere hatoweza kucheza kabla ya mwezi oktoba
kutokana na jeraha la goti.
Cazorla
aliyejiunga na Malaga kutoka klabu ya Villarreal mwaka mmoja tu
uliopita ana urefu wa futi 5 inchi 6 na ameichezea timu ya Taifa ya
Uhispania mwaka 2008 na kwenye mashindano ya Ulaya ya mwaka 2012.
Sahin
alisajiliwa na Real Madrid kutoka Borussia Dortmund kwa mkataba wa
miaka sita mnamo mwezi May 2011 lakini ameshindwa kupata nafasi katika
kikosi Mourinho ambapo kocha huyo ameweza kumruhusu aondoke tu ila kwa
mkopo
SOURCE:http://www.bbc.co.uk/swahili
Post a Comment