Huu ni mkono wa Aunt Ezekiel na hiyo ndio pete aliyovishwa na mchumba wake Dubai.
Stori kamili ni kwamba bado
mpaka sasa movie star wa Tanzania Aunt Ezekiel hajaolewa ila pete ya
uchumba tayari ameshavalishwa kwenye party iliyofanyika huko Dubai, ndoa
ni mwezi november na itafanyika hukohuko Dubai.
Aunt amesema aliemvisha pete ya
uchumba sio mwigizaji wala mtu maarufu wa Tanzania kwa sababu huwa
hapendi kuwa kwenye mapenzi na staa, mumewe mtarajiwa ni Sunday
Demonte…. na anauhakika huyu wa sasa atakua tofauti na mwanaume aliekua
nae 2008/2009 aliekua anampiga na kumnyanyasa kila siku.
Aunt amesema ndoa yake
itakayofungwa Dubai itahudhuriwa na watu 100 tu, amezungumza pia mengine
kuhusu kubadili dini na kufata dini ya mume, kuhamia Dubai pamoja na
ishu nyingine….
chanzo: Millardayo.com
on Wednesday, August 29, 2012
Post a Comment