Kwenye U heard ya XXL Clouds Fm August
28 2012 Gossip Cop Soudy Brown aliripoti kwamba kuna mwanamke
aliekamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa masaa nane wakati akiwa kwenye
mipango ya kumuua msanii wa bongo fleva Ally kiba.
Baada ya kuhojiwa na polisi kwa masaa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.
Alipohojiwa na Soudy Brown, T.I.D alifunguka na kusema “kwa
nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli
sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi
sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo,
kwa sababu gani?
Toka nimezaliwa sijawahi kugombana
na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na
mimi, nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya
nisiuze mziki wangu nisipendwe.”
Soudy alipomtafuta meneja wa Ally Kiba
alijibiwa “hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye
vyombo vya habari sasa hivi lakini ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua”
Post a Comment