Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na familia yao, wakati Rais Kikwete akihojiwa na kujibu maswali kutoka kwa karani wa sensa ya watu na makazi, Clement Ngalaba, Rais alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo lililoanza kufanyika leo Agosti 26, 2012, nchi nzima. PICHA NA IKULU
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akijiandaa kujibu maswali kutoka kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka
(kulia) ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi hilo la Senza ya watu na
Makazi, lililoanza leo nchini kote, ambalo litadumu kwa siku saba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Moahmed Shein, akijiandikisha na familia yake kwa Karani, Asia Hassan Mussa,(kushoto) katika zoezi la Sensa ya Watu na Makaazi, lililoanza leo nchini kote,Rais akiwa katika Shehia ya Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,(kulia ) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein. Picha na Ramadhan Othman,Ikul
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihojiwa na Karani wa sensa, Beatrice Nchimbi wakati alipojiandikisha kijini kwake Kibaoni, mkoani Katavi, Agosti 26,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Post a Comment