Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

VIKOSI VYA RAIS ASSAD VYAFANYA MAUAJI YA KIHISTORIA SYRIA


Vikosi vya majeshi yanayomtii Rais Assad juzi vimedaiwa kufanya mauaji ya halaiki makubwa kuwahi kuonekana tangu kuanza kwa vurugu nchini Syria.
Zaidi ya miili 300, ikiwamo ya wanawake na watoto ilikutwa kwenye nyumba kadhaa. Mingi kati ya hiyo ilikuwa ikionesha imetokana na kuuawa kwa makusudi, wamedai wanaharakati wa upinzani.
Majeshi yanayomtii kiongozi huyo dikteta yamekuwa yakipambana vikali na waasi katika mji wa Darayya, jirani na mji mkuu Damascus. Video kadhaa zimekuwa zikionesha miili iliyotapakaa damu ikiwa imefunikwa kwa mashuka.
Wengi wa waliokufa wanaonekana kuwa ni vijana wa rika la kati lakini angalau video moja imeonesha miili kadhaa ya watoto, ambao wanaonekana wamepigwa risasi kichwani. Mwili wa mtoto mmoja anayeanza kutembea ulikuwa umelala kwenye dimbwi la damu.
"Mauaji ya kimbari", ilisikika sauti ya mtu ambaye anaonekana kupiga picha hizo za video. "Unatazama kulipiza kisasi kwa majeshi ya Assad…zaidi ya miili 150 ikiwa imelala sakafuni kwenye msikiti."
Juzi Waziri wa Mambo ya Nje Alistair Burt alisema: "Nimehuzunishwa mno na taarifa zilizopatikana za mauaji ya kutisha ya halaiki mjini Darayya.
"Ikithibitika, itakuwa ni idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea, na inahitajika kulaaniwa vikali na jamii zote za kimataifa.
"Itaifanya juzi kuwa ni siku ya umwagaji mkubwa wa damu tangu mapigano nchini Syria yaanze Machi 2011, na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 400 kote nchini humo."
Hatahivyo, haikuwezekana kuhakiki kwa uhuru idadi ya miili sababu ya masharti magumu dhidi ya vyombo vya habari visivyo vya kiserikali nchini Syria.
Burt alisema mwendelezo huo umeonesha ipo haja ya kupata msaada wa kimataifa wa haraka kukomesha vurugu.
Urusi na China zimeweka vikwazo vya uchumi kwenye Baraza za Usalama la Umoja wa Mataifa jambo ambalo litaongeza shinikizo kwa vikosi vya serikali.
Uturuki juzi ilianza kwa muda kupokea maelfu ya wakimbizi kwenye upande wa mpaka wa Syria.
Takribani watu 2,000 wameliokimbia vurugu hizo hawakuruhusiwa kuingia Uturuki wakati ikipambana na wimbi kubwa la wakimbizi.
Ofisa alisema: "Hatuna nafasi ya kuwaweka watu wote hawa.
"Tunajitahidi kutengeneza makazi kwanza na yatakapokamilika, tutaruhusu watu hawa kuingia nchini."
Wakimbizi wengi wa Syria nchini Uturuki wameongezeka karibu maradufu zaidi ya ilivyokuwa miezi miwili iliyopita kufikia zaidi ya 80,000.
Kwa ujumla. zaidi ya Wasyria 200,000 wamejazana kwenye nchi jirani mbalimbali tangu kuanza kwa mgogoro huo.
Makamu wa Rais wa Syria, Farouq al-Shara juzi alikutana na ujumbe kutoka Iran mjini Damascus, kumaliza wiki za minong'ono kwamba amejiunga na upinzani.
Alhamisi, vikosi vilirejesha vifaru na helikopta za kivita kutoka Darayya baada ya mapigano yaliyodumu kwa siku kadhaa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top