Wagonjwa wa ebola wakipatiwa matibabu.
Jina la ugonjwa huo, yaani ebola, limetokana na Mto Ebola, uliopo nchini DR Congo.
AINA TANO ZA EBOLA
Zipo aina tano za virusi vya ugonjwa huu na majina yake yamepatikana kulingana na mazingira yake.
Kwa mfano, kirusi cha ebola cha nchini Uganda kinaitwa ‘Bundibugyo Virus’ na kile cha DRC kimepewa jina la ebola.
Kirusi cha nchini Sudan kimepewa jina la Sudan Virus na nchini Ivory Coast kimepewa jina la Tail Virus.
Aina ya tano ya kirusi cha ebola ilipatikana Amerika ya Kusini, lakini kirusi hiki hakijabainika kusababisha madhara kwa binadamu.
Ebola ilivyoingia duniani
Tukio la kwanza la ugonjwa hatari wa ebola liligundulika Agosti 29, 1976 katika eneo la nyanda za juu nchini DR Congo, liitwalo, Yambuku.
Ugonjwa huu uliwapata wakazi wa Yambuku ambao inasemekana walikuwa wakila mizoga ya wanyama wa porini, hasa sokwe na popo.
Mwaka huohuo ugonjwa huo uliibuka nchini Sudan katika maeneo ya viwanda vya pamba, katika Mji wa Nzara na mwaka 1994, ugonjwa huu uliibuka nchini Ivory Coast na kusababisha maafa makubwa.
Ugonjwa wa ebola uliibuka nchini Uganda Julai 2007 katika Wilaya ya Bundibugyo.
Binadamu hupataje ebola?
Utafiti uliofanyika miaka ya nyuma ulibaini kuwa virusi vya ebola huingia kwa mwanadamu kama tulivyosema hapo juu kutoka kwa wanyama wa porini, hasa sokwe na popo.
Baada ya binadamu kula nyama yenye virusi hivyo, husambaa katika mwili wake na huo ndiyo mwanzo wa wanadamu wengine kupata maradhi hayo.
Utafiti huo uligundua kuwa baadhi ya wanyama wanaweza kuishi na virusi vya Ebola bila kuwadhuru wanyama wengine japokuwa wengine huweza kudhurika na kufa kama wanavyoathiriwa wanadamu.
Post a Comment