Mbunge wa Ubungo kupitia
Chadema John Mnyika, amekusudia kuwasilisha mswada binafsi wa sheria ya
marekebisho ya sheria ya sheria za hifadhi ya jamii ya mwaka 2012 kwa
hati ya dharura kwa mujibu wa kanuni ya 81 ya kanuni za kudumu za bunge.
lengo la kuwasilisha muswada
huo ni kufanya marekebisho yenye kuwezesha kurejeshwa kwa fao la kujitoa
ili kuruhusu kuendelea kutolewa kwa mafao kwa mwananchama wa mfuko
husika.
Namkariri akisema “ni vizuri
SSRA wakaeleza kwa ukweli na uwazi pamoja na sababu waliyoitaja ya
kwamba marekebisho haya yalilenga kuhakikisha dhana halisi ya mifuko ya
hifadhi ya jamii watu kupewa mafao inatekelezwa, ni vizuri wakaeleza
ukweli vilevile kwa sababu za ziada za kifungu hiki kuletwa na mazingira
ya kuletwa bila bunge kuelezwa kwa kina, ni vizuri wakatoa taarifa ya
wazi ya sababu za ziada, nasema hivi kwa kurejea ripoti ya mkaguzi mkuu
wa hesabu za serikali za fedha 2010/2011 ambapo maelezo yake yalionyesha
Mkaguzi mkuu anatoa tahadhari kuhusu hali ya mifuko”
Post a Comment