Spika wa Bunge, Anne Makinda, ameunda kamati ndogo ya kuchunguza tuhuma za baadhi ya wabunge kuhongwa na makampuni ya mafuta.
Sakata hilo lilianza baada ya baadhi ya wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2012/13, kudai kuna wenzao wamehongwa na makampuni ya mafuta ili kushinikiza waziri wa wizara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu wake, Eliakim Maswi, wang'olewe katika nafasi zao.
Spika Makinda alitangaza kamati hiyo jana asubuhi baada ya kipindi cha matangazo bungeni.
Alisema ofisi yake imeweka hadidu za rejea kwa kamati ndogo ambazo zinalenga katika kuchunguza na kumshauri kama tuhuma kwa baadhi ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kujihusisha na vitendo vya rushwa ni za kweli ama hapana.
Alisema baada ya mashauriano kati yake na Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan Ngwilizi, ilionekana kuwa kwa kuzingatia uhalisia wa suala lenyewe linaweza kushughulikiwa vizuri zaidi kwa mujibu wa Kanuni ya 114 (18).
Kwa mujibu wa kanuni hiyo, Kamati yoyote inaweza kuunda kamati ndogo kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli zake, kwa kadiri itakavyoona inafaa na kila kamati ndogo itapangiwa kazi zake na kamati ya kudumu inayohusika.
Alisema kamati hiyo itaongozwa na Brigedia Jenerali Ngwilizi kwa lengo la kuwezesha jambo lenyewe kufanya kazi kwa haraka zaidi.
“Kamati hiyo ndogo italifanyia kazi jambo hilo kwa muda wa wiki mbili na baada ya kukamilisha kazi itawasilisha taarifa yake kama Bunge lilivyoamua,” alisema.
Alisema pamoja na Ngwilizi ambaye ni (Mbunge wa Mlalo-CCM), wajumbe wengine ni Kapteni John Chiligati (Manyoni Mashariki-CCM), Riziki Omar Juma (Viti Maalum-CUF), Said Arfi (Mpanda Mjini-Chadema) na Gosbert Blandes (Karagwe-CCM).
“Ili suala hili liweze kushughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi, kamati ndogo inatakiwa kufanya mambo yafuatayo; kwanza ni kukutana na kukubaliana namna bora ya kushughulikia suala hili pamoja na mapendekezo yaliyotolewa,” alisema Spika Makinda.
Aidha, alisema kwa kuzingatia misingi ya haki asilia, katika orodha hiyo hakuna wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini.
Pia alisema mambo mengine ambayo kamati hiyo inatakiwa kuyafanya ni kupitia kumbukumbu rasmi za Bunge za Julai 27 na 28, mwaka huu ambapo bajeti hiyo iliwasilishwa ili kupata picha ya namna mjadala mzima ulivyoendeshwa bungeni.
Spika Makinda aliongeza kuwa mambo mengine ambayo wajumbe wa kamati hiyo wanayotakiwa kuyafanya ni kuwaita na kuwahoji mashahidi ambao wataisaidia kamati kujua ukweli wa tuhuma hizo.
Alimtaja Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, ambaye katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatatu iliyopita alitaja majina ya wabunge kadhaa wenye mgongano wa kimaslahi katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni miongoni mwa mashahidi wanaopaswa kuhojiwa.
Wengine wanaoweza kuwaitwa kuhojiwa ni Waziri wa Nishati na Madini ambaye alibainisha kuwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini walihongwa wakati wa majumuisho ya hotuba yake Jumamosi iliyopita.
“Wabunge wote waliochangia hotuba ya Nishati na Madini na kutoa tuhuma dhidi ya wabunge wengine kujihusisha na vitendo vya rushwa katika wizara hiyo (Nishati na Madini) na mbunge mwingine yeyote anayeweza kuisaidia kamati katika uchambuzi wa suala hili na pia anaweza kuwasilisha taarifa kwa Spika juu ya ushauri na mapendekezo ya hatua zaidi,” alisema Spika Makinda na kuongeza:
“Kamati ndogo hii itashughulikia suala hili katika muda wa siku 14 kwa kuwa ni nyeti na linahusu mustakabali wa Taifa katika suala zima la kupambana na rushwa na vitendo vya rushwa ni muhimu sana. Kamati kwa kadiri inavyowezekana, ijitahidi kuzingatia Katiba, sheria, Kanuni za Bunge na weledi zaidi juu ya suala hili.”
Alisema anamini kuwa wabunge wote ambao walisema kuwa wana ushahidi ama walimtaka Spika ataje majina, sasa watakwenda katika kamati hiyo kutaja majina hayo.
Pia aliwataka wabunge watakaoitwa kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo waitikie wito na kwamba wanaweza kutumia watu wengine wanaofahamu watawasaidia.
Julai 27 na 28, mwaka huu, Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa, aliomba mwongozo kwa kutumia kanuni ya 53(2), 55(3)F na 5 (1) ambapo alisema kuwa michango mingi iliyotolewa na wabunge waliokuwa wakichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, imewatuhumu baadhi ya wabunge kwamba wanajihusisha na vitendo vya rushwa kwa namna moja ama nyingine, wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini.
Baada ya Kawawa kutoa kauli hiyo, Spika Makinda alilipeleka suala hilo katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili tuhuma zifanyiwe uchunguzi na kumshauri Spika ipasavyo.
Chanzo: Nipashe

Post a Comment