Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa
SUALA la mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Malawi na Tanzania,
limezidi kuchukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama kutaka kupewa maelezo juu ya mgogoro huo.
Malawi
na Tanzania zote zilipata uhuru kutoka kwa Uingereza na mipaka
inayotambulika sasa kwa sehemu kubwa, ni ile ambayo iligawanywa wakati
wa Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884/1885.
Hata hivyo, ikiwa sasa ni
takriban muongo mmoja tangu nchi hizo mbili zipate uhuru, Malawi katika
siku za karibuni imeibua mjadala mzito unaotishia uhusiano wa
kidiplomasia na eneo la mpakani na Tanzania, ikisema Ziwa Nyasa lote
liko katika ardhi yake.
Akizungumzia mgogoro huo, Mwenyekiti wa
kamati hiyo,Edward Lowasa alisema baada ya kupata taarifa rasmi ya hali
ilivyo katika mpaka huo, itakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa tamko
lake.
“Tutatoa tamko letu baada ya kupata taarifa rasmi kutoka kwa
vyombo vinavyohusika, kwanza tujue hali ikoje, mambo kama haya hayaendi
haraka,” alisema Lowassa.
Lowassa hakusema taarifa hizo wameomba
kutoka kwenye vyombo gani, badala yake alisisitiza kuwa wametaka vyombo
vinavyohusika kuwapa taarifa rasmi juu ya suala hilo.
Chanzo: Mwananchi
Post a Comment