Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UGUSHI UNASABABISHA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUYUMBA KIUCHUMI KWA ASILIMIA 21



NA  FULLSHANGWE BLOG -ARUSHA

IMEBAINIKA kuwa asilimia 21 ya uchumi wa nchi za Afrika Mashariki kwa
kila mwaka  unayumbishwa na ughushi wa aina mbali mbali ukiwemo wa
luku za umeme ,fedha pamoja na kodi hali ambayo inachangia kiwango
kikubwa cha umasikini

Hayo yameelezwa na Sosthenes Bichanga ambaye ni Mwakilishi  wa Shirika

la Kimataifa la kupambana na ughushi na biashara ya fedha haramu la
Ossulivan Association Kenya, wakati akiongea na waandishi wa habari
mapema jana jijini Arusha.

Alisema kuwa kiwango hicho cha fedha ambazo zinapotea kwa kila mwaka

kinasababishwa na sababu mbalimnbali ndani ya nchi hizo za Afrika ya
Masharikii mara baada ya kufanyika utafiti wa siri katika maeneo ya
nchi hizo, ambapo kwa sasa wamejipnga kuhakikisha kuwa wanatoa elimu
zaidi hasa elimu ya Kiuasibu ili kukwepa hasara hizo.,

Pia alisema kuwa zoezi hilo la kugushi fedha hasa kwenye  Taasisi za

Fedha pia zinatokana na elimu finyu ambayo wananchi wanayo hivyo kuna
umuhimu mkubwa kwa wakaguzi na wahasibu kupatiwa mbinu mbali mbali za
kuthibiti hali hiyo


“Tafiti zilizofanyika zinaonyesha mamlaka mbali mbali za mapato ya

nchi za afrika yanavamiwa na wataalamu wa kughushi na hatimaye
wanajikuta wanaletewa nyaraka zinazoonyesha kuwa kodi imelipwa na
wanapotazama mfumo wa ndani wa mawasiliano malipo yanakuwa hayajaingia
huu ndio ughushi tunaotaka kuuthibiti kwa wale wanaofanya
hivyo”alisema Bichang”

Aliongeza kuwa hali hii ya juu ya kiugushi wa kieletroniki

imesababisha hasara kubwa ndio maana makampuni mengine ya umeme
hayajitoshelezi kwani yanajipanga kupata faida na mwisho wa siku
yanaishia kupata hasara

Kutokana na hali hiyo ya ughushi shirika hilo limeandaa kongamano

litakalofanyika wiki ijayo mjini hapa  kwa ajili ya kutoa  mbinu za
kiuasibu za kuchunga na kukagua fedha, ambapo watu elfu nne
watahudhuria wakiwemo maafisa wa tra,maafisa wa benki,maafisa ugavi wa
umeme,wahasibu,maafisa wa takukuru,wakaguzi wa mahesabu pamoja na
wakurugenzi wa mashirika.

Awali mwakilishi wa kongamano hilo kwa mjini hapa Solomon Njiamoja

alisema kuwa wahasibu na wakaguzi wanapaswa kutumia fursa hiyo ya
kujifunza mbinu mbali mbali za kupambana na ughushi ili waweze
kuthibiti wizi unaotokea mara kwa mara
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top