![]() |
Simba SC |
Na Mahmoud Zubeiry
KATIKA
kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii, mabingwa wa Tanzania Bara, Simba
SC, Jumamosi watacheza mechi ya kujipima nguvu na Mathare United ya
Kenya kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Habari za ndani kutoka Simba, ambazo BIN ZUBEIRY
imezipata, zimesema kwamba tayari makubaliano yamefikiwa na timu timu
hiyo ya Daraja la Kwanza Kenya, ambayo ilimuibua kisoka mshambuliaji wa
AJ Auxerre ya Ufaransa, Dennis Oliech.
Simba
itamenyana na Azam katika mechi ya Ngao ya Jamii ya kuashiria
kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Septemba 8,
mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Habari
za ndani kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimesema kwamba,
kuchelewa kwa mechi hiyo ambako kumeenda sambamba na kuchelewa kuanza
kwa ligi hiyo, kumetokana na kuchelewa kufikiwa mwafaka mapema wa
mkataba mpya wa udhamini wa Ligi Kuu.
Mkataba
wa awali wa Vodacom na TFF unafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu na
kusainiwa mkataba mwingine, baada ya majadiliano yanayoendelea.
Lakini
kwa kuwa Mkutano Mkuu wa TFF uliopita uliridhia kuanzia msimu ujao
Ligi Kuu iendeshwe na kampuni itakayoundwa na klabu za Ligi Kuu mjadala
kuhusu udhamini mpya wa ligi umekuwa mrefu kutokana na kuhusisha pande
tatu, klabu, wadhamini na shirikisho.
Lakini
sasa, kwa vyovyote, hata maridhiano ya mkataba mpya wa udhamini na
Vodacom yachelewe tena, mechi hiyo itachezwa Septemba 8, ikiwa ni wiki
moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
Kihistoria
hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili
kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba
na Yanga.
Mtibwa
ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao
2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya
Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao
kihistoria.
Katika
mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi
Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka
jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga
Yanga mabao 2-0. KWA HISANI YA BIN ZUBEIRY BLOG
MABINGWA WA MECHI ZA NGAO YA JAMII:
Mwaka Mshindi Matokeo
2001 Yanga 2-1 Simba
2010 Yanga 0-0 Simba (3-1penalti)
2011 Simba 2-0 Yanga
Post a Comment