Mwanamuziki
aliyejiunga na Twanga Pepeta akitokea bendi ya Mapacha Watatu, Kalala
Junior akiimba nyimbo yake mpya Nyumbani ni Nyumbani wakati
wa mkutano wa kumtambulisha kwa waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Kiongozi wa bendi hiyo, Saleh Kupaza.Kwa hisani ya
Habari Mseto Blog
DAR ES SALAAM,Tanzania
UONGOZI
wa kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET)
umemtambulisha rasmi mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Kalala Hamza
Kalala maarufu kwa jina la Kalala Junior.
Kalala
alitambulishwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
kwenye ukumbi wa Mango Garden ambapo mbali ya kusema kuwa amerejea kwa
lengo la kuendeleza bendi yake hiyo aliyokuwa nayo kabla ya kujiunga na
Mapacha Watatu.
Mwimbaji
huyo maarufu alisema kwa fumbo kuwa “Koti limembana akiwa na bendi
yake ya Mapacha na kuamua kulivua na kuacha kuendelea kulivaa tena” na
kujiunga na Twanga.
“Nimefurahi
kujiunga na Twanga tena na nimekuja na zawadi za nyimbo mbili, wimbo
wa kwanza unaitwa Nyumbani ni Nyumbani ambao kwa sasa upo katika hatua
ya mwisho na utatambulishwa rasmi wiki ijayo, ni wimbo ambao
unazungumzia mambo mbali aliyokutana nayo katika muziki mpaka kuamua
kurejea Twanga,” alisema Kalala.
Alisema
kuwa ujio wake wa Twanga siyo wa kulazimishwa, bali umetokana na
mapenzi yake mwenyewe na hasa akikumbuka fadhira za ASET ambapo ndipo
alipata umaarufu mkubwa.
“Nawaomba
wadau wa Twanga wakae mkao wa kula, kwani nimerejea kivingine na
watarajie kupata mambo mengi mazuri, nitafanya zaidi ya yale
niliyoyafanya zamani, lengo ni kuendelea kushika hatamu katika muziki
wa dansi,” alisema Kalala ambaye vionjo vyake ‘vimewashika’ mashabiki
wengi wa muziki wa dansi.
Afisa
Habari wa ASET, Mohamed Pizaro alisema kuwa ujio wa Kalala umetokana
na mpango wao waliouanzisha ujulikano Amsha Amsha Twanga Pepeta
Nyumbani ni Nyumbani .
Pizaro
alisema kuwa mpango huo ni maalum kwa kuhimarisha bendi yao na hasa
kwa wanamuziki ambao wameonyesha nidhamu nzuri wakiwa chini ya ASET na
sasa wanatumikia bendi nyingine.
Kiongozi
msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza alimpokea kwa mikono miwili
mwimbaji huyo na kusema kazi ya kujihimarisha zaidi imeanza.
“Karibu
nyumbani, si unajua nyumbani ni nyumbani, tunaamini hata hao wengine
wanajifanya vichwa ngumu, nao watarejea tu,” alisema Kupaza
chanzo: Kamanda wa Matukio
Post a Comment