KIKOSI CHA YANGA
Mabingwa
wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (KAGAME) timu ya
Young Africans Sports Club iliyokuwa imeweka kambi ya wiki moja nchini
Rwanda kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu, itashuka
dimbani kucheza na Coastal Union ya Tanga siku ya jumamosi Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz
Afisa Habari wa klabu ya Yanga Louis Sendeu amesema watatumia mchezo
huo kama sehemu ya maandalizi ya ligi kuu nchini, inayotazamiwa kuanza
mwezi septemba.
Young
Africans iliyokuwa nchini Rwanda kwa muda wa wiki moja, ilicheza
michezo miwili ya kujipima nguvu na timu za Rayon Sports na Police Fc.
Katika
mchezo wa kwanza, Young Africans iliifunga Rayon Sports mabao 2- 0,
mabao yaliyofungwa na Saimon Msuva na Hamis Kiiza, huku mechi ya pili
dhidi ya Police Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, mabao yakifungwa
na Nadir Haroub 'Cannavaro' na Stephano Mwasika.
Timu
ilirejea siku ya jumatatu kutoka Kigali Rwanda na jana iliendelea na
mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola ambapo inaendelea na
mazoezi kila siku asubuhi kwa kipindi hichi chote cha maandalizi ya
ligi kuu.
Aidha
mchezaji mpya kutoka APR FC ya nchini Rwanda, mlinzi Mbuyu Twite
anataajiwa kuwasili kesho majira ya mchana saa 9, akitokea nchini Rwanda
alipobakia kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuja nchini na familia
yake.
Mbuyu
Twite anawasili kesho mchana kwa shirika la ndege la Rwanda Air akiwa
sambamba na mjumbe wa kamati ya utendaji Abdallah Bin Kleb aliyekua
amebakia pia nchini Rwanda kuhakikisha Twite anakamilisha zoezi hilo.
Viiingilio vya mchezo dhidi ya Coastal Union siku ya jumamosi ni:
VIP A, 20,000/=
VIP B & VIP C , 10,000/=
Orange, 5,000/=
Blue & Green 3,000/=
Wapenzi,
wanachama na washabiki wa Young Africans mnaombwa kujitokeza kwa wingi
siku ya jumamosi Uwanja wa Taifa , itakua ni fursa ya kuwaona wachezaji
wote waliosajili msimu huu.
Post a Comment