DMX kapanda on air tena na kumchana rapper Drake ambae siku kadhaa zilizopita alirekodi kolabo na sauti ya marehemu Aaliyah.
Kwenye interview na Power 105,
Dmx amesema msimamo wake bado uko palepale kwamba sio shabiki wa Drake,
alipoulizwa kuhusu album mpya ya Aaliyah ambayo Drake ni producer mkuu,
DMX ameshtuka na kusema hiyo ni kumkosea Aliyah heshima, kama
wamemdharau na hakubaliana na hiyo ishu.
Imempa hasira DMX na kusema
anatamani wakati huu ungekua miaka 7 iiyopita, unakutana na mtu kwenye
lift unampiga alafu unasepa, Drake hawezi kuendelea kuachiwa kufanya
mambo ya kipuuzi kama hayo.
Baada ya hiyo kauli, mtangazaji
alimwambia Dmx kwamba ni ngumu kumkuta Drake anatembea bila walinzi
hivyo hatoweza kupata nafasi ya kumpiga, Dmx akajibu “hata mimi natembea
na washkaji zangu pia”
Post a Comment