1.Uwajibikaji
wa kisiasa wa viongozi wa serikali na idara zake.,Waziri Emmanuel
Nchimbi,IGP Mwema,Paul Chagonja,RPC Morogoro na Kamanda wa FFU,na RPC
IRINGA na Kamanda wa FFU wajiuzulu na au wafukuzwe kazi
2.RPC Morogoro na Iringa,makamanda wa FFU Morogoro na Iringa,na maaskari waliouwa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka
3.Rais
aunde tume huru ya uchunguzi wa vifo tata katika matukio ya
kisiasa.1.ARUSHA vifo 3.IGUNGA,vifo vingi havijulikani bado,3.ARUMERU
MASHARIKI,vifo 5, 4.SINGIDA kifo 1, MOROGORO na IRINGA
chadema haitatambua wala kushirikiana na kamati batili ya NCHIMBI.
4.Msajili
wa vyama vya siasa John Tendwa ni mtu hatari kwa taifa kwa kauli tata
anazozitoa.anashirikiana na au anajipendekeza kwa CCM na Serikali
yake.CHADEMA tangu sasa haitafanya kazi na Tendwa wala kufanya
mawasiliano naye ya kiofisi.Labda kama atagundua makosa yake na kuomba
msamaha,chadema itatafakari namna ya kufanya naye kazi tena.
5.TBC
TAIFA Television na Redio ni hatari kwa taifa,kwa kubobea kupotosha
umma juu ya matukio mengi.Hivyo CHADEMA Inatangaza mgogoro na TBC na
inaelekeza na kuomba wanachama ,wapenzi,na wananchi wote wapendao ukweli
na haki,kuisusia TBC
6.Jeshi
la Polisi lijue kuwa Maandamano ndiyo siasa yenyewe na mikutano ya
hadhara ni lazima kwa mawasiliano ya umma na siasa.kuzuia vitu hivyo ni
kunyima wananchi haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kukusanyika na kutoa
maoni,pia kupata habari na taarifa
7.Operesheni
MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba ilivyopangwa
katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si
nyingi.Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo
singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki na baiskeli
na miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo mengine,Chadema
wanasema kwa sababu maalum katika jimbo hilo watapita kitongojikwa
kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya viongozi (msisitizo ni wa msoma
MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri ya
wanahabari waliokuwepo)
8.Kutokana
na mgogoro wa muda mrefu mkoani mwanza uliosababisha meye wa chadema
kuvuliwa umeya kinyume na utaratibu na kwa njama za CCM na Serikali,na
bahati mbaya sana kwa kushirikisha madiwani wa CHADEMA,KAMATI KUU
imewavua UANACHAMA madiwani wake wawli 1 ADAMU CHAGULANI wa kata ya
IGOMA na HENRY MATATA wa KITANGIRI, PIA uongozi wote wa CHADEMA mkoa wa
mwanza Umevunjwa.
Post a Comment