* WAAPA KUTOKURUDIA TENA KUGOMA KWA MASLAHI YA WATU WACHACHE
MADAKTARI wanaofanya kazi chini ya usimamizi wa madaktari bingwa (interns), ambao walisimamishwa wakati wa mgomo wa madaktari wamejitokeza na kuomba radhi kwa wananchi na serikali kwa kushiriki migomo na kusababisha madhara makubwa kwa baadhi ya wananchi.
Madaktari hao ambao walikusanya saini zaidi ya 200 kutoka kwa wenzao, walienda mbali zaidi na kuapa kwamba hawako tayari kushiriki tena kwa namna yoyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya wananchi.
Kwa kauli hiyo ni dhahiri kwamba madaktari hao wamemgeuka kinara wa migomo ya madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, ambaye ni Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Nchini.
Dk. Ulimboka ambaye amepata umaarufu mkubwa kwa kuongoza migomo hiyo, hivi karibuni alinusurika kifo baada ya kutekwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Pande na watu wasiojulikana na baadaye kwenda kutibiwa nchini Afrika Kusini.
Mwingine ambaye alikuwa akiongoza migomo hiyo ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi, ambaye hivi sasa amefunguliwa mashtaka ya kuhamasisha migomo hiyo iliyoleta athari kubwa nchini kwa wagonjwa wengi kupoteza maisha kwa kukosa matibabu.
Akizungumza na wandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam jana Kiongozi wa Madaktari hao, Dk. Paul Swakala, alisema kuwa ushiriki wao wa mgomo wakati ule ulikuwa hauepukiki.
“Ingawa utamaduni wa kuomba radhi hadharani katika nchi yetu haujazoeleka, tumeamua kufanya hivyo kwa sababu sisi ni binadamu na binadamu wote tuna upungufu.
“Tunaomba radhi kwa Rais Jakaya Kikwete na serikali yake kwa usumbufu uliosababishwa na mgomo ule kwani tunatambua jitihada zake za kutafuta suluhu ya mgomo ule,” alisema.
Alisema wanatambua na kuunga mkono juhudi za Rais Kikwete katika kuboresha huduma za afya nchini na changamoto nyingi zinazoikabili sekta hiyo nchini.
Alisema wanamuomba aiangalie zaidi sekta ya afya kwani maisha ya Watanzania wengi yanategemea huduma bora za sekta hiyo nyeti.
Kiongozi wa kundi hili la madaktari alienda mbali zaidi kwa kuwaomba radhi wananchi wote hasa wale waliokumbwa moja kwa moja na madhara yaliyosababishwa na migomo ile ambayo ushiriki wao kwa wakati ule ulikuwa hauepukiki.
“Tunawaomba radhi wananchi wote walioathirika na mgomo ule, tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea kwani tunajua kwamba wananchi wengi walichukizwa na migomo hiyo.
“Kwa hakika, tunajutia sana kosa hili na tuko tayari kurejea kazini kuendelea kuwahudumia Watanzania wenzetu kwa moyo mweupe,” alisema.
Madaktari hao wametoa ombi kwa Rais Kikwete la kutaka kuonana naye ili waweze kuomba radhi kwake ana kwa ana.
Machi saba mwaka huu, madaktari walitangaza mgomo wa bila kikomo wakimtaka Rais Kikwete amtimue madarakani aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya.
Hata baada ya Rais Kikwete kuwatimua vigogo hao, mgomo huo uliibuka tena huku madaktari wakidai pamoja na mambo mengine, nyongeza kubwa ya mshahara pamoja na stahiki zao nyingine.
Mgomo huo ulimalizika baada ya serikali kutishia kuwafukuza kazi madaktari wote waliogoma huku Rais Kikwete akitamka wazi kwamba serikali yake haina uwezo wa kulipa kima cha chini cha mshahara cha sh milioni tatu kilichopendekezwa na madaktari hao.
CHANZO: TANZANIA DAIMA

Post a Comment