Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SURUHISHO LA MIGOGORO YA VYUO VIKUU VYATAJWA

NAFASI ya demokrasia katika serikali za wanafunzi na umuhimu wa kuendelezwa kwa ujuzi wa uongozi kwa wanafunzi hao vimetajwa kuwa kati ya vitu muhimu kumaliza migogoro katika vyuo vikuu na kujenga viongozi bora wa kitaifa siku zijazo.
Haya yapo katika mada kuhusu serikali za wanafunzi na demokrasia katika vyuo vikuu iliyotolewa katika kongamano la nne la elimu ya juu lililomalizika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.
Mada hiyo ilitayarishwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Utawala na Fedha, Profesa Faustine Kamuzora pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Utawala, Profesa Yunus Mgaya.
“Maswala hayo ni muhimu hasa wakati huu wa ushindani mkubwa katika dunia,” alisema Profesa Kamuzora ambaye aliwasilisha mada hiyo katika kongamano hilo lililotayarishwa na kamati ya Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu na Wakuu wa Vyuo nchini Tanzania (CVCPT) kwa kushirikiana na taasisi ya Trust Africa.
Profesa Kamuzora alisema kama vyuo vikuu vinataka kufikia malengo yake, ikiwa ni pamoja na kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi, havina budi kufanya mipango ya kuendeleza mbinu za uongozi, kujiamini na kujitegemea kwa wanafunzi wao kuwa miongoni mwa ajenda zao kuu.
“Hii ni kwa sababu viongozi wengi wa wanafunzi huishia kuwa viongozi katika jamii zao baadaye na hivyo kuna kila sababu kuhakikisha viongozi hawa wa wanafunzi wanafuata miiko ya uongozi inayotakiwa katika vyuo vyao,” alisema.
Akitoa mfano alisema baadhi ya waliokuwa viongozi wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wametokea kuwa viongozi katika Chama cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF).
Awali, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa changamoto kwa wadau wote wa elimu ya juu nchini kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja na kufikia malengo yanayotegemewa.
Washiriki wa kongamano hilo la siku mbili, walikuwa pamoja na wenyeviti wa mabaraza ya vyuo vikuu, makamu wakuu wa vyuo vikuu, wakuu wa vyuo, manaibu wakuu wa vyuo wa vyuo vyote vya serikali na vya umma, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) na wadau wengine wa elimu ya juu kutoka ndani na nje ya nchi.

chanzo: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top