Mhe. Waziri na ujumbe wake wakiwa katika maonyesho ya Sekta ya usafiri wa Anga mjini Berlin.
Mhe. Waziri na ujumbe wake wakiwa katika Majadiliano na Uongozi wa Sekta ya Usafiri wa Anga, Germany
Mhe. Waziri akiwa ndani ya moja ya ndege iliyokuwepo katika maonyesho hayo.
Mhe. Waziri akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa ndege za Airbus, nchini ujeruman (hayupo pichani) pembeni yake ni Mhe. balozi wa tz Berlin.
**********************************************
Mhe. Waziri na ujumbe wake wapo Berlin kuanzia trh 15 hadi 19 sept, 2012. moja ya tukio muhimu ni kusainiwa Mkataba wa Ushirikiano wa Usafiri wa Anga (Bilateral Air Services Agreement - BASA) baina ya nchi hizi mbili tarehe 17 Sept. Aidha, leo tarehe 16 sept, Mhe. Waziri na ujumbe wake walitembelea maonyesho ya Kimaitaifa ya sekta ya Usafiri wa Anga yaliofanyika hapa Berlin. Aidha kwa nyakati mbalimbali, Mhe. na ujumbe wake watakutana na wafanyabiasha na wawekezaji mbalimbali hususani katika sekta ya usafiri (Anga, reli na meli).Endele kufuatilia blog audiface jackson kupata mengi zaidiBaada ya ziara ya hapa ujeruman, ujumbe wa wataalam (tu) aliofatana nao mhe. waziri utaelekea the Hague Uholanzi kwa ajili ya majadiliano mengine kuhusu usafiri wa anga tarehe 19 hadi 21 sept. Mhe waziri hatushiriki.
Post a Comment