Kanisa kuu katoliki jimbo la Bukoba ambalo masalia ya marehemu kardinali Rugambwa yatazikwa ndani yake.
Kanisa katoliki nchini
dayosisi ya Bukoba mkoani Kagera, wanajiandaa kuzika upya masalia ya
mwili wa aliyekuwa askofu wa dayosisi hiyo Kardinali Laurean Rugambwa,
aliyefariki mnamo mwaka 1997 katika kanisa kuu la Bukoba. Maziko ya
Kadinali Rugambwa yamepangwa kufanyika siku ya oktoba 6 mwaka huu.
Mwili wa askofu huyo wa kwanza nchini na Kardinali wa kwanza
mweusi barani Afrika umezikwa katika kanisa la kwanza mkoani Kagera
lililopo Kashozi kutokana na kwamba kanisa kuu la Bukoba ambalo marehemu
aliagiza kuzikiwa ndani yake lilikuwa katika matengenezo makubwa.
Akizungumza katika kipindi cha Baragumu Channel ten na
baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,
Askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba Askofu Methodius Kilaini , amesema
wanataka kumzika kardinali Rugambwa kwa heshima tena katika kanisa
alilopenda kuzikiwa kutokana na kukamilika kwake, lakini kabla ya
kuzikwa humo kutatanguliwa na ibada mbalimbali ikiwa sehemu alikozaliwa,
alikobatizwa, sherehe zitakazoambatana na kusherehekea miaka 100 ya
kuzaliwa kwa kardinali Rugambwa tarehe 7 mwezi Octoba.
“tuna alika watu wengi
kuhudhuria kwenye tukio hili…, na pia tunakaribisha michango
itakayowezesha kuwa na kitu cha kumkumbuka marehemu kwa mchango wake….
alisema askofu Kilaini.
Naye mmoja wa wajumbe wa kamati
ya maandalizi ya kufanikisha tukio hilo , James Rugemalira, alimwelezea
Kardinali Rugambwa kama mtu aliyetoa mchango mkubwa kwenye jamii ya
watanzania, kuanzia kwenye nyanja za elimu, afya na kiroho.
Marehemu Kardinali Rugambwa ana
mambo mengi ya kukumbukwa na jamii ya watanzania hususani watu wa mkoa
wa Kagera hasa kwa juhudi zake za kupeleka elimu mkoani humo kwa kuagiza
ujengwaji wa shule za msingi na sekondari ikiwemo shule ya kwanza ya
wasichana ya Rugambwa ambayo ujenzi wake ulikuwa ni mafanikio ya
marehemu huyo kuomba msaada wa ujenzi wa shule hiyo alipohutubia bunge
la Ujerumani akiwa mwafrika wa kwanza.Licha ya mambo
hayo yote kanisa hilo pia liko mbioni kuanzisha mfuko rasmi wa kumuenzi
kardinali huyo mfuko utakaojulikana kwa jina la Kardinali Rugambwa ambao
utakuwa maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.
Padre Laurean Rugambwa aliwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 10 Februari,1952.
Alizaliwa julai 22 1912 na kufariki miaka 15 iliyopita.
chanzo:Fullshangweblog
Post a Comment