 |
Kaimu
meneja Tawi la NMB Mbalizi road John Chinguku akimkabidhi tani moja ya
mifuko ya sementi mshindi wa promosheni ya jenga maisha yako na NMB Bi
Akson Sheyo Mwinga huku Meneja NMB kanda ya nyanda za juu Lucresia
Makiriye pamoja na watumishi wengine wakishuhudia tukio hilo la utoaji
zawadi hizo |

 |
Baadhi ya washindi wa promosheni ya jenga maisha yako na NMB wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao
Jenga
Maisha Yako na NMB ni promosheni iliyoanzishwa na NMB baada ya kugundua
kuwa watanzania wengi wana matarajio na malengo wanayotaka kuyatimiza
maishani, kama vile; kumiliki nyumba nzuri, kusomesha watoto shule nzuri
na mambo mengine mazuri.
NMB
inapenda kuwasaidia watanzania wote ili kuhakikisha wanafikia ndoto zao
katika maisha waliojipangia, hivyo basi ndipo NMB ikaja na msingi wa
kuzifikia ndoto hizo unaojulikana kwa jina la Jenga Maisha Yako na NMB.
Jenga Maisha Yako na NMB ni
promosheni iliyounganishwa na akaunti za NMB Junior akaunti na NMB
Bonus akaunti. Promosheni hii itawaingiza moja kwa moja wateja
waliofungua NMB Bonus akaunti au NMB Junior akaunti wenye kiwango
kisichopungua shilingi 50,000 au kinachozidi hapo ili kushinda zawadi
mbalimbali.
|
on Saturday, September 15, 2012
Post a Comment