Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATAKA LUGHA ZA ALAMA KWA WAGONJWA

 

.

WATOA huduma za afya na maafisa maendeleo ya jamii kutoka wilaya za Bahi na Chamwino mkoani Dodoma wameiomba Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuweka mitaala ya lugha za alama kwa wanafunzi wanaosomea uuguzi ili waweze kukabiliana na changamoto ya kuwahudumia wagonjwa wenye ulemavu wa kusikia.
Ombi hilo lilitolewa jana na watoa huduma za afya kwenye mkutano ulioandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata), mkoa wa Dodoma, uliojadili changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wakati wa kupata huduma za afya hasa VVU na ukimwi.
Walisema changamoto kubwa inayowakabili katika kazi yao ni kuwahudumia viziwi kwa kuwa wengi wao hawajui kuongea na hivyo kufanya mawasiliano baina yao kuwa magumu pindi wanapofika katika vituo vya afya kupata huduma.
Walisema kuwa endapo serikali itaweka mitaala ya kufundisha lugha za alama kwa viziwi kwenye vyuo vyote vinavyotoa wahudumu wa afya nchini kwa kiasi kikubwa viziwi watakuwa wameweza kukabiliana na changamoto hiyo ya mawasiliano.
“Inatuwia vigumu pale wanapokwenda hospitali wakati wanaumwa na kuwepo mkalimani pembeni kwani wanakosa uhuru wa kuzungumza uhalisia wa ugonjwa kwani magonjwa mengine ni siri kati ya daktari na mgonjwa,” alisema mmoja wao huku wengine wakiitikia.
Wakichangia katika mkutano huo watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) walisema kuwa mawasiliano baina yao na watoa huduma za afya ni changamoto kubwa ambayo inawakabili watu wenye ulemavu huo kwa kuwa hakuna siri kati yao na mtoa huduma kwani hulazimika kuwepo kwa mkalimani wa lugha baina yao.
Walisema kuwa kama serikali itasikia kilio chao na kutoa mafunzo ya lugha za alama kwa watoa huduma ya afya, masuala yao yatabaki kuwa siri na kwamba chama cha viziwi Tanzania, wilaya ya Bahi, na Chamwino wako tayari kutoa mafunzo ya alama bure kwa watoa huduma wote wa afya ili angalau wawepo wachache wa kuwasiliana nao.
chanzo: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright 2025 EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG | Designed By Code Nirvana
Back To Top